Masanduku maalumu kwa ajili ya uwekaji wa kura yakiwa yameandalia kwa ajili ya wajumbe wa mkutano mkuu wa Jimbo la Hai kumhagua kada atakaye peperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu unatarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu
Msimamaizi wa Uchaguzi katika jimbo la Hai Kataba Sukuru akizungumza wakati wa zoezi la utangazaji wa matokeo katika uchaguzi huo .
Mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya na Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ni miongoni mwa wajumbe walioshiriki katika kufanya uamuzi wa kumpata kada atakaye peperusha bendera ya Chama hicho.
Baadhi ya Wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Hai wakiwa katika maandalizi ya zoezi la upigaji kura.
Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya akiwa amebeba karatasi ya kura tayari kwenda kumchagua kada atakaye peperusha bendera katia jimbo la Hai.
Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya akipiga kura yake.
Lengai Ole Sabaya akitumbukiza kura yake katika sanduku la kura.
Wajumbe wakiwa katika foleni ya kwenda kupiga kura.
Baadhi ya wagombea wakingojea maamuzi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Hai wa nani atawavusha katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu .
Huyu ni Saashisha Mafuwe Mshindi wa kura za maoni katika jimbo la Hai .
Mgombea wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Hai ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Saashisha Mafuwe akiwa amebebwa juu mara baada ya kutangazwa mshindi wa kura za maoni ambapo wajumbe walimpigia kura 124
Na Dixon Busagaga ,Hai
Mgombea ubunge katika jimbo la Hai katika kura za maoni za
Chama cha Mapinduzi (CCM) na kada wa chama hicho Saashisha Mafuwe ameibuka
mshindi baada ya kupigiwa kura 124 na wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo hilo.
Hatua hiyo ni hitimisho la chaguzi za ndani ya Chama cha Mapinduzi za kura za maoni katika ngazi ya majimbo
ambapo majimbo manne kati ya tisa ya mkoa wa Kilimanjaro yalikuwa yamesalia
baada ya zoezi hilo kuanza siku Jumatatu.
Majimbo yaliyokuwa yamesalia katika uchaguzi uliofanyika
Jumatatu ni pamoja na jimbo la Moshi vijijini,Jimbo la Hai na Jimbo la Same
Magharibi .
Katika uchaguzi wa jimbo la Hai Mafue ambaye ni mtumishi
kati tume ya madini amewashinda aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Hai Fuya Kimbita aliyepata kura 85 akifuatiwa na
Abubakar Msangi aliyepata kura 48 kati
ya wagombea 42 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.
Katika Jimbo la Moshi vijijini wagombea walikuwa ni 47
waliorejesha fomu huku wagombea 46 wakijitokeza kuwania nafasi hiyo ,mpambano
mkali ukikua baina ya Prof Patrick Ndakidemi,Deogratius Mushi na Moris Makoye .
Msimazmizi wa uchaguzi katika jimbo la Moshi mjini Asia
Halamga akamtangaza Profesa Patrick Ndakidemi kuwa mshindi baada ya kuibuka kura
262 akiwashinda Deogratius Mushi aliyepata kura 46 akifuatiwa na Moris Makoi .
Katika jimbo la Same Magharibi ,Mbunge anayemaliza muda wake
Dkt Mathayo David ametetea nafasi yake baada ya kupata kura 389 dhidi ya kura
300 za mshindani wake aliyemfuatia Angela Kairuki huku nafasi ya tatu
ikishikiliwa na Marry Mgonja aliyepata kura 18.
Hatua ya awali ya uchaguzi katika majimbo ya mkoa wa
Kilimanjaro umemalizika huku majina ya walioshika nafasi za juu yakitaraji
kupelekwa katika vikao vya Chama cha
Mapinduzi kwa ajili ya mapendekezo na maamuzi .
Chama cha Mapinduzi kwa sasa kinajielekeza katika Chaguzi za
kura za maoni kwa Wabunge watakaotokana na viti maalumu zoezi linalotarajia
kufanyika siku ya Alhamisi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇