“Nimefurahi kuwaona Marais Wastaafu, nimefurahi kumuona Mama Anna Abdallah huyu Mama alinifundisha Kazi lakini pia alimfundisha kazi Mwinyi akiwa Naibu Waziri wa Afya, nimefurahi kumuona Mzee Kinana, Lowassa, Mzee Sumaye, Maspika Wastaafu na wote” -JPM
“Mambo yaliyofanyika ni mengi, kila mmoja ni shahidi, hata Viongozi wa Vyama vya upinzani wanafahamu mazuri yaliyofanyika hata Nchi jirani wanafahamu, Ndege 11 kununuliwa kwa mpigo tena kwa cash,Elimu bure, Barabara,vituo vya afya nyinyi wote ni mashahidi”-JPM
“Tumeipeleka Nchi kwenye uchumi wa kati, tumepambana vizuri na corona na mengine mengi, tumeitengeneza Tanzania, ni mafanikio yetu wote hata ambao hawako CCM na ndio maana Mzeee Mrema mapema kabisa akasema yeye hana mgombea Urais, mgombea wake CCM maendeleo hayana chama” - JPM
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇