LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 3, 2020

RAIS MAGUFULI ATEUA WAKUU WAWILI WA MIKOA NA TISA WA WILAYA WAPYA, ANDENGENYE NDANI.

Rais Dk. John Magufuli
Ikulu, Chamwino
Rais Dk. John Magufuli leo Julai 3, 2020 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa wawili na wakuu wa wilaya tisa wapya.

Taarifa ya Ikulu imesema,  Rais amemteua Dk. Philemon Sengati kuwa Mkuu wa mkoa wa Tabora aliyewahi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.


Wakati kabla ya uteuzi huo, Dk. Sengati alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza na kuchukua nafasi  Aggrey Mwanri ambaye amestaafu Andengenye anachukua nafasi ya Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga ambaye pia amestaafu.

Taarifa hiyo imesema Wakuu tisa wa wilya walioteuliwa na Rais Magufuli ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Ismail Twahir Mlawa ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro na kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Morogoro na anachukua nafasi ya  James Mugendi Ihunyo ambaye naye amestaafu. 

Mwingine ni Jamila Yusuf ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi na kabla ya uteuzi huo, alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma na anachukua nafasi ya Lilian Charles Matinga ambaye pia amestaafu.

Rais Magufuli amemteua pia Mhandisi Martine Ntemo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mhandisi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na anachukua nafasi ya Asumpter Nshunju Mshama ambaye amestaafu.

Salum A. Kali ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza na kabla ya uteuzi alikuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza na anachukua nafasi ya Dk. Philemon Sengati ambaye katika uteuzi huo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Taarifa imesema Rais Magufuli amemteua Wilson Samwel Shimo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Mkoani Geita, kabla ya uteuzi huo, alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida.

Wengine ni Kanali Mathias Kahabi ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera, anachukua nafasi ya Saada Malunde ambaye amestaafu.

Abbas Kayanda aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha, kabla ya uteuzi huo, alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu na anachukua nafasi ya Theresia Jonathan Mahongo ambaye amestaafu.

Lazaro Jacob Twange anayekuwa Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara anachukua nafasi ya Elizabeth Simon Kitundu ambaye amestaafu.

Wa tisa ni Toba Alnason Nguvila aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni na kabla ya uteuzi alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Longido Mkoani Arusha, anachukua nafasi ya Godwin Gondwe ambaye amehamishwa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, kuchukua nafasi ya  Felix Jackson Lyaniva ambaye amestaafu.

Taarifa hiyo ya Ikulu, imesema uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 03 Julai, 2020 na wateule wote wanatakiwa kuwepo Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 06 Julai, 2020 saa 4:00 asubuhi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages