LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 8, 2020

MBUNGE WA ZAMANI WA CHADEMA JOSHUA NASSARI ATINGA CCM ARUSHA

Mbunge wa zamani wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chadema Joshua Nassari, akizungumza baada ya kupokewa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika  Ofisi ya CCM mkoa wa Arusha.

KAULI ZAKE SABA BAADA YA KUJIUNGA NA CCM

Joshua Nassari aliyewahi kuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo July 8 2020 kwenye ukumbi wa CCM Arusha ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM ambapo hizi hapa chini ni kauli zake saba miongoni mwa mengi aliyoyazungumza;-

“Wengine wanasema Nassari anautaka Ubunge, niwaambie sijatangaza nia mahali popote na sijaja CCM kutangaza nia, nimetafakari na pia Jamii, Wazee wa Meru na Marafiki waliofanya nikawa Mbunge mdogo kuliko wote Nchi hii wameniambia, naona CCM huku kunafaa”

“Haikuwa kazi rahisi kufanya haya maamuzi ya kuja CCM, yale yote mnayotaka kuyasikia na kuyaona kutoka kwangu mtayasikia na kuyaona hata kama sio leo, sababu kubwa iliyonileta CCM ni kwakuwa naipenda Nchi yangu”

Joshua Nassari leo Arusha
“Ukiongea habari ya Ndege.. Wapingaji wanasema nani anapanda? mbona wakati wa Mwl. Nyerere hamkusema Mwl. unatupa Ndege hatuna hela ya kupanda, leo tuna Ndege 11, ile moja ni USD Mil 31, nimeingia Bungeni hatuna hata Ndege, unaachaje kumuunga mkono JPM!?”

“Nimeamua kuiweka Nchi yangu mbele, najua wapo watakaonitukana watakaosema hili na lile kisa mimi kuhamia CCM lakini sitojali, nawashukuru Watu wa Meru kwa kuniamini kwa mihula miwili mfululizo nikiwa Mbunge mdogo kuliko wote Tanzania”

“Watanzania wanaokwazwa kwa kuona nimeingia CCM ambao walitamani kuendelea kuniona upinzani naomba mnisamehe, siwezi kuendelea kuwa mnafiki roho yangu imekataa, sijatangaza nia na huenda nisichukue fomu, mkisema tunataka tukupe sehemu hayo tutaongea baadaye”


“Yako mengi tutayazungumza huko mbele, nilichagua kuingia kwenye siasa ili kuijenga Nchi ndio maana nilichimba visima, nilinunua vitanda Hospitali, sasa yote ambayo nilikuwa napigania JPM ameyafanya nikimpinga nitaonekana sina akili”


“Siku zote nafanya siasa za kiungwana, nimeshawaandikia barua CHADEMA na kiukweli naishukuru CHADEMA ilinichukua nikiwa mdogo wakanisikiliza wakaona kuna potential ndani yangu, nawashukuru kwa kunilea nitakuwa mjinga kama sitoikumbuka historia

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages