Makada 69 wa CCM wamechukua fomu za kuomba kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Akizungumza na mwandishi wa makala hii ofisini kwake katibu wa CCM wilaya ya bagamoyo Getruda Bonifasi Sinyinza amesema idadi hiyo ni hadi kufikia saa 10 jioni siku ya tarehe 16 ikiwa ni siku ya tatu tangu zoezi hilo la kuchukua fomu lilipozinduliwa rasmi nchini kote ndani ya Chama cha Mapinduzi.
Getruda amesema wilaya ya Bagamoyo ina majimbo ya uchaguzi mawili yaani jimbo la Bagamoyo na jimbo la Chalinze ambapo jimbo la Bagamoyo wanaCCM 44 wamejitokeza kuchukua fomu na wanaCCM 25 wamejitokeza kuchukua fomu kugombea ubunge jimbo la Chalinze wakati kati yao tisa ni wanawake.
Aidha katibu hiyo wa CCM wilaya ya Bagamoyo amewataka wote waliochukua fomu kugombea kuzingatia sheria na taratibu za Chama pamoja na taratibu na sheria za nchi kwani vyombo vya usalama vipo macho kuwafuatilia nyendo zao.
Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo Getruda Sinyinza akimkabidhi fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya Ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Bagamoyo Hassan Kiangio leo 16 julai 2020
Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo Getruda Sinyinza akimkabidhi fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya Ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Chalinze Patricia Kizigo leo 16 julai 2020
Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo Getruda Sinyinza akimkabidhi fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya Ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Bagamoyo Charles Godfrey Makoba leo 16 julai 2020
Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo Getruda Sinyinza akimkabidhi fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya Ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Bagamoyo Mkufunzi wa Chuo cha Diplomasia kurasini Dr. Ahamad Mtengwa Burnan leo 16 julai 2020
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇