MADIWANI wapya sita wa Viti Maalumu kwenye Tarafa 7 zilizopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wamechomoza katika kura za maoni zilizofanyika Julai 27 wilayani hapa.
Madiwani hao wanaungana na waliotetea nafasi zao wanaotoka Tarafa za Miono, Kwaruhombo, Chalinze na Mwambao kulikokuwa na diwani mmoja mmoja, ambapo kwa sasa Mwambao na Chalinze mbali ya waliotetea nafasi zao pia wameongezwa mmoja hivyo kuwa na Madiwani wawili.
Chini ya Usimamizi Juma Gama Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoani hapa akisaidiwa na Katibu wa (CCM) Gertrude Sinyinza, UWT iliwakilishwa na Hanipha Checheta Katibu na Lukhia Masenga Mwenyekiti wa Jumuia hiyo ukishuhudiwa na Kamati ya Siasa wilaya ikiongozwa na Mwenyekiti Abdul Sharifu.
Tarafa ya Yombo sura mpya zilizoingia ni Veronica Ndetiyai kura 275 na Ummy Kisebengo 387 wakiwashinda waliotetea nafasi hizo Togo Omary 76 na Elizabeth Shija 77, wakati Mwambao sura mpya Sinasud Onelo 498, akiungana na aliyetetea Shumina Rashid 464.
Tarafa ya Miono Sijali Mpwimbwi akiibuka tena katika nafasi hiyo kwa kura 449 dhidi ya Esther Helman 84, Tunu Mpwimbwi 421 amerejea Tarafa ya Kwaruhombo, huku Mwanakesi Madega 381 aking'ara Chalinze akiunga na sura mpya Tatu Mpogo 278, wakimuongoza Upendo Moreto 197.
Tarafa ya Msata Anzeni Rajabu amepata kura 297 akimshinda mgombea mwenzake Amin Hamisi 185, wakati Tarafa ya Msoga Debora akimshinda Zaytuni Kaoka 132.
Baada ya zoezi hilo Gama aliwaambia wajumbe hao kuwa kwenye zoezi hilo hakuna mshindi, kwani majina yote yatasubiri vikao vya ngazi za juu vitavyokuja na maamuzi ya nani ataipeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi wa mwezi Oktoba.
Akihitimisha mchakato huo, Masenga aliwashukuru wagombea kwa kuthubutu, sanjali na wajumbe huku akuwaomba waendelee kuungana ili kuhakikisha chama hicho kinaibuka na ushindi kwenye uchaguzi Mkuu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇