LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 6, 2020

INDIA YAPIGA MARUFUKU NYAMA YA MBWA

 Nyama ya mbwa yapigwa marufuku katika mkoa wa NagalandKaskazini-Mashariki mwa India.

India  yapiga marufuku nyama ya mbwa katika  mkoa wa Nagaland , mkoa ambao unapatikana Kaskazini Mashariki mwa  India.

Kulingana na taarifa ziliztolewa katika jarida la The Indian Express ni kwamba  katibu wa jimbo la Temjen Toy nchini India  amesema kwamba serikali imechukuwa uamuzi wa kupiga marufuku  biashara ya nyama ya mbwa kwa hali yeyote.

Nyama mbwa ilikuwa ikiliwa kitamaduni katika majimbo ya Kaskazini-Mashariki mwa India.

Baadhi ya  mashirika ya kiraia katika maeneo hayo yamekemea uamuzi  huo wakati ambapo shirika la kimataifa la haki za wanyama  limepongeza uamuzi huo uliochukuliwa na serikali.

Zaidi ya mbwa  30 000  kila mwaka   huuzwa  katika  masoko  ya  majimbo hayo ambayo  yana utamaduni wa kula mbwa Kaskazini-Mashariki mwa India.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages