LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 10, 2020

HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA (NEC) ILIVYOMRIDHIA DK. MWINYI KUMRITHI DK. SHEIN URAIS ZANZIBAR


Aliyekuwa Mgombea wa kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk. Hussein Mwinyi akipunga mkono baada ya Wajumbe wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kumchagua kuwa mgombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, katika Kikao hicho kilichofanyika leo katika Ukumbi wa jengo la White House, Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma leo. Nyuma ni Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally.

CCM Blog, Dodoma
Hatimaye jibu la kile kitendawili kilichokuwa likisubiriwa kwa hamu cha kumpata Mgombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa October mwaka huu wa 2020, leo limepata baada ya Chama Cha Mapinduzi kumempitisha Dk. Hussein Mwinyi kuwa Mgombea Urais wa kiti hicho.

Husein Mwinyi amepatikana baada ya Wajumbe wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kumchagua  kwa kura 129 sawa na asilimia 78.65 ya kura zote zilizopigwa kwa wagombea wote watatu waliofikishwa kwenye Kikao hicho baada ya kupitishwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM katika kikao kilichofanyika jana.

Katika kinyang'anyiro hicho, Dk. Mwinyi aliingia amechuana na wagombea wengine wawili ambao ni Dk. Khalid Salum Mohamed na Waziri Kiongozi wa zamani wa Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha.


“Wote hawa watatu ambao tutawapigia kura ili kumpata mmoja wanafaa ila yupo mmoja anayefaa zaidi ni jukumu lenu kumchagua anayefaa na nina matumaini kati ya hawa mmoja atakuwa Rais wa Zanzibar
Tusichukiane, mimi niliomba kura na Mzee Pinda na nikampindua, Makongoro Nyerere na wengine ila leo tupo hapa, kazi hizi ni kazi za kupita, wagombea wote 31 nawapongeza kwa kuchukua fomu atakayepita mmoja tumuunge mkono, saa nyingine maneno yanaletwa na upinzani na CCM tunayabeba” alisma Dk. Magufuli

















.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages