LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 15, 2020

MAKADA BUKOBA WAPIGANA VIKUMBO KUCHUKUA FOMU ZA KUOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA UBUNGE

Na Allawi Kaboyo, Bukoba
Baada ya Chama Cha Mapinduzi (ccm) kutangaza kuanza kwa mchakato wa kuwapata wagombea wake kwa nafasi za Ubunge, Udiwani, Uwakilishi na Viti Maalum kuanza kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya Chama kugombea nafasi hizo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, leo Julai 14, Makada mbalimbali wamefurika katika ofisi za CCM Wilaya ya Bukoba mjini Mkoani Kagera kuchukua fomu za kuomba ridhaa hiyo ya kugombea Ubunge jimbo la Bukoba Mjini.

Miongoni mwa waliofika katika ofisi hizo na kuchukua fom ni wakili msomi Aaron Kabunga ambaye ni mwenyekiti wa chama cha mawakili wa kujitegemea kanda ya Kagera ambaye amesema kuwa licha ya kuwa yeye ni wakili laki pia ni mwanachama hai wa chama hicho hivyo baada ya kujipima ameona anatosha kuwatumikia wanabukoba mjini kupitia ubunge.
Ameeleza kuwa msimu huu chama kimewapa nafasi kila mwananchama anayejua anatimiza vigezo kugombea nafasi yoyote ikiwa ni demoklasia hivyo ameona anayohaki ya kuchukua form na kugombea na matumaini yake ni kwamba chama kikimpitisha basi ataweza kuipeperusha vyema bendera katika uchaguzi mkuu.
“Nimefika hapa kuchukua fom kwaajili ya kuomba nafasi ndani ya chama change kuipeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya ubunge wa jimbo la Bukoba mjini, ni imaani yangu fomu hii nitaisoma na kuielewa na baadae nitaijaza na kuirudisha, lengo langu ni kuwatumikia watanzania wa Bukoba mjini hivyo nikishukuru chama kwa kutupa nafasi wanachama wote.” Amesema wakili Kabunga.
Kabunga amesema kuwa mambo ni mengi ya kuifanyia Bukoba ni mengi na anayo malengo makubwa kwaajili ya Bukoba kwakuwa kwa miaka mitano jimbo hilo lilikuwa upinzani na sasa ni muda wa kulikomboa.
Wengine waliochukua fomu ni mfanyabiashara maarufu Audax Kaijage maarufu Omujumba ambaye pia aliwahi kuwa diwani kwa kipindi kilichopita ambaye kasema kuwa lengo ni kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Bukoba mjini.
Bi Cristine Rwezahula ni mwanamke ambaye nay eye amejitosa katika kinyanganyiro cha kuwania kuipeperusha bendera ya CCM kwa nafasi ya ubunge jimbo la Bukoba mjini ambapo amesema kuwa anaamini chama kimewapa nafasi kubwa wananwake katika nafasi za utawala hivyo ameona anafaa kugombea ubunge katika jimbo hilo.
Ameongeza kuwa wanawake ni jeshi kubwa katika chama chao hivyo kama chama kimewaamini sasa hawana sababu za kusita kugombea nafasi za uongozi na kuwatumikia watanzania.
Mwingine ni aliyekuwa katibu wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Kagera Bukoba Ndg.Kilwanila Kiiza, Ndg. Valeriani Rugarabamu na wengine wengi ambao hadi saa saba mchana waliochukua fomu walikuwa wamefikia Zaidi ya wagombea 20 kwa jimbo la Bukoba mjini.

 Wakili msomi Aaroni Kabunga ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mawakili wa Kujitegemea Kanda ya Kagera akipokea fomu ya kuwania kugombea Ubunge Jimbo la Bukoba mjini kutoka kwa Kaimu katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Bukoba mjini Editha Domician ambaye ni Katibu wa UVCCM wilaya ya Bukoba mjini.

 Mfanyabiashara maarufu Audax Kaijage (Omujumba) kushoto, akipokea fomu ya kuwania kugombea ubunge jimbo la Bukoba mjini kutoka kwa Kaimu katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Bukoba mjini  Editha Domician ambaye ni Katibu wa UVCCM wilaya ya Bukoba mjini.
 Kilwanila Kiiza aliyekuwa Katibu wa Hospitali ya Rufaa mkoa Kagera, akiwa ameshikilia fomu ya kuwania kugombea ubunge wa jimbo la Bukoba mjini baada ya kukabidhiwa
 Bibi Cristine Kagemulo Rwezahula (kushoto) akipokea fomu ya kuwania ubunge jimbo la Bukoba mjini kutoka kwa Kaimu katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Bukoba mjini Editha Domician, ambaye ni Katibu wa UVCCM wilaya ya Bukoba mjini.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages