LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 25, 2020

WANACHAMA WA CCM 2688 WAJITOKEZA KUMDHAMINI RAIS MAGUFULI MKOA WA KUSINI UNGUJA

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja wajitokeza kumdhamini Mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli, hafla hiyo imefanyika Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, kama wanavyoonekana pichani wakiwa katika mstari wakisubiri kumdhamini Mgombea wao.
Na. Maelezo  Zanzibar 25/06/2020.
Wanachama 2688 wa Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja wamejitokeza   kumdhamini mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk,John Pombe Magufuli ambae anagombea awamu ya pili katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Akitoa ufafanuzi katika zoezi hilo liliofanyika Ofisi za Chama Dunga Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, Katibu  wa Chama cha Mapinduzi  Mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Mzee Charas amesema zoezi hilo ni muhimu katika maendeleo ya Chama.
Alisema miongoni mwa wana CCM waliojitokeza kumdhamini Dk Magufuli  ni pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu, Umoja wa Vijana (UVCCM), Jumuiya ya wanawake, viongozi wa Mitaa, pamoja na wananchi wa kawaida.
Akizindua zoezi hilo, Mwenyekiti wa Chama Cha Maapinduzi Wilaya ya Kati Hassan Mrisho Vuai amewapongeza wanachama wa CCM kwa kujitokeza kwa wingi  kumdhamini DK.John Pombe Magufuli.
“Tuna  kila sababu ya kumdhamini na kumkubali Dk John Pombe Magufuli kutokana na kazi nzuri alizozifanya katika kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano ili arudi kuendeleza kazi hizo kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania,” alisisitiza Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kati
 Aidha alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa jitihada kubwa aloifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo, na kuwataka wananchi kuzidi kuyathamini Mapinduzi, rasilimali za nchi na kuuthamini uhuru wao.
Nae Mkuu wa Wilaya ya kati Bi. Hamida Mussa Khamis amesema Serikali inaunga mkono  harakati hizo na kuwahakikishia ulinzi, usalama na amani katika  wilaya hiyo ili kutumikia chama kwa usalama kwa lengo la  kuimarisha demokrasia.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages