LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 6, 2020

UN: RAIA 1,300 WAMEUAWA DRC, JINAI ZA KIVITA ZIMETENDEKA

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema takribani watu 1,300 ambao ni raia wameuawa katika matukio tofauti yanayohusisha makundi ya watu wenye silaha na vikosi vya serikali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC katika kipindi cha miezi minane iliyopita.
Kwa mujibu wa taaifa hiyo iliyotolewa Ijumaa mjini Geneva Uswisi, baadhi ya matukio hayo yanayohusisha mauaji, ukatili na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu huenda yakawa ni jinai dhidi ya binadamu au jinai za kivita.
Taarifa hiyo imebaini kuwa idadi ya waliokumbwa na ukatili huo imeongezeka katika wiki za hivi karibuni wakati machafuko yakishika kasi kwenye majimbo matatu ya Mashariki mwa DRC ya Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini.
 Ofisi ya haki za binadamu inasema makundi yenye silaha yamefanya mauaji makubwa na uhalifu mwingine na majeshi ya ulinzi na usalama pia yamehusika katika ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu katika majimbo hayo matatu lakini pia katika sehemu zingine nchini humo.
Kamisha mkuu wa ofisi ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet
Akizungumzia hali hiyo Kamisha mkuu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amesema “Nimeshtushwa na kuongezeka kwa mashambulio ya kikatili dhidi ya raia wasio na hatia yanayofanywa na makundi yenye silaha.” Aidha amesema ameshtushwa na  ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na vikosi vya ulinzi na usalama yakiwemo mauaji na unyanyasaji wa kingono. Ameongeza kuwa kwenye jimbo la Ituri kwa mfano kati ya Oktoba Mosi 2019 na Mei 31 2020 raia 531 waliuawa na unyama mkubwa ulitendeka ukiwemo ukatili wa kingono na watu kukatwa vichwa na maiti za watu kukatwa vipandevipande na pande zote za makundi yenye silaha na jeshi la Congo FARD na polisi wa nchi hiyo PNC pia wakilaumiwa kuhusika.
Nako Kivu Kaskazini ofisi ya haki za binadamu inasema raia 514 waliuawa kati ya Novemba 2019 na Mei 31 mwaka huu likihusishwa jeshi la wapiganaji wa ADF, jeshi la serikali FARD na jeshi la polisi wa congo la PNC.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages