LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 20, 2020

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM NA AHADI ZA MBUNGE JIMBO LA MAKETE 2015-2020

Prof. Norman Adamson Sigalla King, Mb (2015-2020)

Show quoted text

Mfuko ulianzishwa kwa sheria namba 16 ya mwaka 2009 iliyotungwa na bunge na kupitishwa tarehe 21 Agost 2009. Mfuko utaitwa Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo - Constituencies Development Catalyst Fund (CDCF).
Lengo la mfuko huu ni miradi ya maendeleo kwenye kila jimbo la Uchaguzi, kwa hiyo itapokea fedha na kuchangia kwenye miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Jimbo  kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya miradi hiyo.
Fedha ya mfuko inatolewa na serikali kuu kila mwaka wa fedha kulingana na Mpango na Bajeti ya Jimbo/Halmashauri ya Wilaya husika. Katika kipindi cha miaka 4 mfuko umetekeleza shughuli/miradi kama ifuatavyo:-
  1. Mwaka 2015/16 zilipokelewa jumla Tshs. 33,812,000.00; mfuko ulichangia (kwa kuchangia bati 1,160, mchanga trip 23 na saruji mifuko 280)  katika miradi ya:-
  • Ujenzi wa zahanati 2 (Ihela, Ilevelo na Makeve),
  • Ukamilishaji waVyumba vya madarasa 9 katika shule za msingi za Kisaula, Lugoda, Ruaha, Malembuli, Maleutsi, Manga, Mwera, Kidope na Mkondo B Igofi Kinyika,
  • Ujenzi wa ofisi za kata 2 za Mlondwe na Kigala,
  • Ukamilishaji wa mabweni 3 katika shule za sekondari za Makete Girls, Mwakavuta na Kipagalo,
  • Ukamilishaji wa Bwalo katika sekondari ya Lupila na Ujenzi wa maabara 3 katika shule ya sekondari ya Isapulano.
  1. Mwaka 2016/17 zilipokelewa jumla Tshs. 29,608,959.00; mfuko ulichangia upatikanaji wa vifaa katika miradi; vifaa hivyo ni saruji mifuko 500, bati 1,015 na  Mchanga trip 4 katika miradi ya:-
  • Ujenzi ofisi 2 ya Kigala na Kijiji cha Makeve,
  • Ujenzi wa daharia 3 katika shule za sekondari Makete Girls, Lupalilo na Mount Chafukwe,
  • Ujenzi wa zahanati 4 za Ugabwa, ukwama, Ludihani na Uganga,
  • Ujenzi wa vyumba vya madarasa 7 katika shule za msingi za Nkenja, Kiduga, Kilimani, Bulongwa, Lugoda, Igenge na Mbela,
  • Ujenzi wa Bwalo 1 na Maafa Isapulano bati 160.
  1. Mwaka 2017/18 zilipokelewa jumla ya Tshs. 36,080,000.00 mfuko ulichangia upatikanaji wa vifaa katika miradi; vifaa hivyo ni saruji mifuko 690, bati 1,130 na  Mchanga trip 12, madawati 50 na Samani za zahanati ya Mago katika miradi ya:-
  • Ukamilishaji wa zahanati 9 za Malembuli, Kitula, Malembuli, Usungilo, Mago, Ilevelo, Unyangogo, Mang’oto na Nhungu,
  • Ukarabati na umaliziaji wa vyumba vya madarasa 14 katika shule ya Kisasatu, Manga, Tandala, Igolwa, Ikuwo, Imehe, Ludihani,  Unyangala, Utengule, Mahulu, Ipelele Mkondo B, Mount Chafukwe sekondari na Ipepo Sekondari,
  • Vikundi vya wanawake 10 vya Iniho, Lupalilo, Iwawa, Ujuni, Ilindiwe, Ludilu, Mbalatse, Bulongwa, Isapulano na Ikuwo,
  • Ujenzi ofisi 9 Kigulu, usagatikwa, kimani, mfumbi, Kisinga, Tandala, Usililo, Kigala, na Utengule,
  • Kusaidia upatikanaji wa madawati 50 Isapulano sekondari na
  • Ujenzi wa maabara 3 kinyika sekondari.
  1. Mwaka 2018/19 zilipokelewa jumla ya Tshs. 34,282,000.00 mfuko ulichangia upatikanaji wa vifaa katika miradi; vifaa hivyo ni saruji mifuko 450, bati 1,382 na  Mchanga trip 10, Photocopier machine na Kikundi cha wanawake Lupalilo; katika miradi ya:-
  • Vyumba vya madarasa 13 katika shule za Kidope, Mago, Ukwama, Usalimwani, Ulumba, Uganga, Imehe, Idende na Ng’onde,
  • Ujenzi wa nyumba 5 katika shule ya Kiduga, Makangarawe, Ikete, Uganga na Kisasatu,
  • Ujenzi wa jengo 1 la utawala katika shule ya sekondari ya Mlondwe,
  • Ujenzi wa ofisi 4 Kigala, Madihani, Ikete na Ndapo,
  • Ujenzi wa zahanati 2 ya Ihela na Masisiwe na
  • ujenzi wa daharia 2 katika sekondari za Mang’oto na Makete Girls.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages