Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akizungumza na watendaji na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo katika kikaokazi ikiwemo kutoa maelekezo ya kukamatwa kwa watendaji kwa tuhuma za tubadhilifu wa fedha sh. milioni 307 za umma.
Na Allawi Kaboyo, Biharamulo.
Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewaagiza Kamanda wa Polisi na Kamanda wa TAKUKURU mkoani Kagera kuwakamata watumishi 34 katika Halmashauri ya wilaya Biharamulo wakiwemo watendaji wa vijiji na kata kwa kushindwa kurejesha sh. milioni 307 zilizokusanywa kutoka vyanzo vya mapato ya ndani bila kupelekwa Benki.
Agizo hilo amelitoa leo alipofanya ziara ya kikazi wilayani humo kutoa maelekezo ya kiutendeji kutokana na Halmashauri hiyo kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato na kuonekana kuna ubadhilifu wa fedha za serikali.
Mkuu huyo licha ya kuagiza kukamatwa na kuwekwa chini ya ulizi watumishi hao, ameziagiza Mamlaka kuwasimamisha kazi Kaimu Mweka Hazina Sospiter Makene, Jastine Banula Ofisa Tehama, Rogers Semukoko afisa Tehama na Beatrice Gurusya Ofisa Biashara wote wakiwa ni watumishi wa Halmashauri hiyo.
Gaguti amechukua uamuzi huo baada ya kutoa siku saba kwa watumishi hao kurejesha fedha hizo kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo kilichofanyika juni 05 mwaka huu kilichokuwa kina lengo la kujibu hoja za Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali.
“Nilikuja hapa nikatoa maelekezo kwa wale wote waliokuwa wanakusanya fedha kwa kutumia mashine za Poss bila kuzipeleka benki kuwa warejeshe fedha na nikawapa siku 7, lakini fedha iliyorejeshwa ni asilimia 2%.
Kwa mwendo huu hatuwezi kwenda lazima tuweke misingi imara ya kuboresha utumishi na uadilifu, hapa nina orodha ya watendaji 30 ambayo nampati kamanda wa polisi kuhakikisha watu hao wanakamatwa popote walipo na wengine wane hawa naagiza wasimamishwe kazi lakini wawe chini ya uangalizi wa kamati ya ulizi na usalama ili kutoa ushirikiano.” Amefafanua RC Gaguti.
Ameongeza kuwa watumishi wa umma wanatakiwa kuwa waadilifu na kuiogopa fedha ya serikali na kuahidi kuwachukulia hatua wote watakao bainika wakifanya vitendo vya ubadhilifu na kutoa onyo kali kwa watendaji wa vijiji na kata mkoani humo kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali bila kuleta ujanjajanja.
“Fedha ya serikali ni ya moto hivyo haipaswi kulala niwasihi tu ndugu zangu tusijaribiane, hatutasita kumchukulia hatua yeyote atakayehusika na upotevu wa pesa, tambueni watendaji ndiyo mnadhamana ya kukusanya mapato ya ndani kutoka katika vyanzo vya mapato katika maeneo yenu.” Ameeleza Gaguti.
Aidha Gaguti amesema kuwa kuna baadhi ya watumishi walikataa kusajili vyanzo vya mato kwa makusudi na baadae kuwarudi wafanyabiashara na kuchukua fedha kinyemela na kusababisha serikali kukosa mapato yake.
Your Ad Spot
Jun 23, 2020
Home
featured
Kitaifa
RC KAGERA AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI WATUMISHI WANNE NA WATENDAJI WENGINE 30 KUKAMATWA WILAYANI BIHARAMULO KWA UBADHILIFU WA SH. MILIO 307.
RC KAGERA AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI WATUMISHI WANNE NA WATENDAJI WENGINE 30 KUKAMATWA WILAYANI BIHARAMULO KWA UBADHILIFU WA SH. MILIO 307.
Tags
featured#
Kitaifa#
Share This
About Bashir Nkoromo
Kitaifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇