Pierre Nkurunziza |
Rais Dk. John Magufuli ametangaza maombolezo ya Kitaifa ya siku tatu kuanzia kesho Juni 13, 2020 kufuatia kifo cha Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza kilichotokea Juni 09, 2020 nchini Burundi.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu jijini Dodoma imesema katika kipindi chote cha siku tatu za maombolezo hayo ambayo yataanza leo, hadi keshokuwa bendera zote zitapeperushwa nusu mlingoti.
Taarifa hiyo imesema, Rais Magufuli ameeleza kuwa Tanzania inatoa heshima hiyo kwa kifo cha Pierre Nkurunziza kwa kutambua kuwa alikuwa Rais wa nchi jirani ambayo imekuwa na uhusiano na ushirikiano mzuri wa kirafiki, kihistoria na kidugu na Tanzania.
“Burundi ni mwanachama mwenzetu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Rais Nkurunziza aliipenda Jumuiya hii, pia aliipenda Tanzania na alishirikiana nasi kila ilipohitajika, hivyo nimeona Watanzania tuungane na ndugu zetu wa Burundi katika kuomboleza na kumkumbuka Rais Nkurunziza ambaye aliiona Tanzania kama nyumbani kwake” Taarifa hiyo imemnukuu Rais Magufuli akisema.
"Rais Magufuli amerudia kutoa pole kwa Mjane wa Rais Nkurunziza, Mama Denise Bucumi Nkurunziza, Familia, Serikali na Wananchi wote wa Burundi kwa kuondokewa na mpendwa wao, na amemuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina", imemalizia taarifa hiyo.
Nitumie nafasi hii kushukuru Chama changu Cha CCM kupitia M/Kiti Taifa Mh.John Pombe Magufuli kwa kutambua mchango mkubwa wa Pierre Nkurunziza katika kudumisha amani ktk jamii ya Burundi na Afrika sanjari na upeo wake mkubwa katika masuala ya kidplomasia,hakika tumepoteza Giant man ktk jamii ya Afrika .Pia niendelee kuiomba serikali yangu ya CCM kuendelea kutoa ushirikiano wa kidplomasia kwa Burund kwa minajali ya kudumisha amani na mshikamano na kuendelea kuondoa dhana za ukabila ktk taifa hilo.@Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Pierre mahali pema@SHEDRAKA P.KAGIYE,Katibu Hamasa na Chipukizi UVCCM(KAKONKO).
ReplyDelete