LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 3, 2020

RAIS DK. MAGUFULI ATETA NA RAIS DK. SHEIN, MANGULA NA DK. BASHIRU ALLY, IKULU YA CHAMWINO, DODOMA, LEO

Rais Dk. John Magufuli na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mohamed Ali Shein, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi-Bara Mzee Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru  Ally wakiwa katika kikao cha ndani  katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, leo.

CHAMWINO, Dodoma
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. John Magufuli amekutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein katika kikao cha ndani kilichofanyika Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma, leo.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti CCM Bara Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally ambapo viongozi hao wamezungumzia masuala ya CCM.

Baada ya kikao hicho, Rais Dk. Shein amekwenda kuweka udongo katika jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za Ikulu na kukagua maendeleo ya kazi ya ujenzi wa ofisi hizo inayofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia shirika lake la Suma JKT.

Rais Dk. Shein amemshukuru Rais Dk. Magufuli kwa kumpa fursa ya kwenda kuweka udongo ikiwa ni kumbukumbu ya ujenzi wa ofisi hizo na amebainisha kuwa kujengwa kwa ofisi hiyo ni heshima kwa Taifa na tafsiri sahihi ya kujitawala.

“Huko ndio kujitawala, kutawaliwa sio kuzuri, mtawala anafanya anavyotaka yeye, anafanya kwa utashi wake pale anapotaka yeye kufanya,

 Tunapochukua hatua ya kujitawala wenyewe tunafanya mambo makubwa kama haya kwa ajili ya wananchi, hii ofisi ni ya wananchi wa Tanzania” amesema Rais Dk. Shein.

Rais Dk. Shein amewasalimu vijana wa JKT wanaofanya kazi za ujenzi wa ofisi hizo na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya na amewataka kujivunia fursa hiyo adhimu ya kujenga ofisi ya Ikulu za nchi yao, badala ya kazi hiyo kufanywa na kampuni za nje ya nchi kama ambavyo hufanyika katika maeneo mengi. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na  Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mzee Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru  Ally Kakurwa wakifuraia jambo leo tarehe 03-06-2020 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein Ikulu ya Chamwino   Dodoma leo. 

 Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein akiangalia kibao cha jiwe la msingi la Ujenzi wa Uwekaji Ofisi za Ikulu ya Chamwino.
 Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein akiangalia akiweka udongo katika jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za Ikulu na kukagua maendeleo ya kazi ya ujenzi wa ofisi hizo inayofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia shirika lake la Suma JKT.

 Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein akizungumza na wajenzi kutoka JKT mara baada ya kukagua kazi za Ujenzi wa Ofisi za IKULU

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages