Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dk. Maulid Banyani
Nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Iyumbu mkoani Dodoma.
NA MWANDISHI MAALUMSHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) ni moja ya mashirika ambayo ni nguzo ya Serikali ya Awamu ya Tano katika uteketezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), inayoliongoza taifa kuelekea kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Mwandishi maalum ambaye amekuwa akimulika mwenendo wa utendaji wa taasisi na mashirika ya umma, amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dk. Maulid Banyani kuhusu utekelezaji wa majukumu ya shirika hilo analoliongoza katika kipindi cha takriban miaka mitano ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano na kuibuka na mambo kadhaa.
Mazungumzo hayo yalifanyikia ofisini kwa Mkurugenzi huyo Mkuu, Barabara ya Ufukoni, Upanga Jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita, Dk. Banyani alianza kwa kugusia kidogo historia ya shirika hilo, sababu za msingi zilizomsukuma Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kulianzisha na jinsi linavyotekeleza majukumu yake ya kuwapatia Watanzania makazi bora.
"Historia ituhukumu kwa matendo yetu, sisi NHC nina hakika historia itasomeka kuwa tumefanikiwa sana kuilinda ndoto za Mwalimu Nyerere za kuanzishwa kwa shirika hili ambazo Rais John Pombe Magufuli ameapa kuzitekeleza kwa vitendo.
Ieleweke kwamba Shirika la Nyumba la Taifa lilianzishwa mwaka 1962, kwa Sheria ya Bunge namba 45, lengo likiwa ni kuwapatia wananchi makazi bora.
Hili ndilo Shirika la kwanza kuanzishwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mwaka mmoja tu baada ya uhuru wa nchi yetu na hii ni kwa sababu Mwalimualiamini kuwa malazi bora ni moja ya vitu vitatu muhimu katika maisha ya mwanadamu." anasema Dk. Banyani na kuongeza;
"Kwa hiyo hili ni shirika muhimu sana na lina dhamana kubwa katika ustawi wa jamii yetu. Sasa tangu kuanzishwa kwa NHC, limekuwa katika safari ndefu ya kuleta mageuzi kwenye sekta ya nyumba.
Katika kipindi cha miaka minne na nusu ya Serikali ya Awamu ya Tano, Shirika hili limeendelea kutekeleza majukumu yake ya ujenzi wa nyumba za kuuza na kupangisha, usimamizi wa nyumba na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya serikali na taasisi zingine kama mkandarasi."
"Serikali ya Awamu ya Tano inapoelekea kutimiza takriban miaka mitano madarakani ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (2015/16 hadi 2019/2020), shirika limetekeleza jumla ya miradi 94 ya nyumba za makazi na biashara na kati ya hiyo, iliyokamilika ni miradi 53.
Kwenye miradi hii iliyokamilika, zaidi ya nyumba 1100 za gharama nafuu zimejengwa katika Halmashauri za Wilaya mbalimbali na zaidi ya nyumba 6100 zimejengwa kwa watu
wa kipato cha kati kwa ajili ya makazi na biashara." Anasema Dk. Banyani.
Anasema, Shirika lilianzisha na linaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa miji ya pembezoni, ikiwemo Kawe wenye ukubwa wa ekari 267 na Burka Materves Arusha wenye ukubwa
wa ekari 579. na kwamba Miji hii ya pembezoni inalenga kupunguza msongamano katikati ya miji yetu kwa kuwa inakusudiwa kuwa na mahitaji yote muhimu.
Kwa mujibu wa Dk. Banyani, ujenzi wa miradi hii mikubwa na midogo unalenga kuchangia utatuzi wa tatizo la uhaba wa nyumba nchini unaokadiriwa kufikia nyumba 3,000,000 pamoja na kukuza mchango wa sekta hiyo kwenye pato la Taifa.
"Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 iliyonadiwa na Rais John Magufuli inalitaka shirika kujenga nyumba kuwapatia
wananchi makazi bora na nafuu.
Katika utekelezaji wa Ilani, kwetu sisi NHC dhamira yetu ni kuwa na kasi kubwa ya ujenzi wa nyumba. Katika kipindi hiki cha miaka minne na nusu, niseme sasa wananchi wameweza kununua nyumba tulizojenga
kupitia mikopo ya benki washirika ambazo tuna makubaliano nazo.
Benki hizi ni pamoja na Benki ya Azania, Bank of Africa, Benki ya CRDB, Benki ya Exim, Benki ya KCB, Benki ya NBC, Benki ya DCB, Commercial Bank of Africa, Benki ya
NMB, Banc ABC, NIC na Benki ya Stanbic.
Nyingine ni First National Bank (FNB), International Commercial Bank (ICB) na Diamond Trust Bank (DTB)." anasema Dk. Banyani.
Anasema, kupitia mpango huo, wananchi wengi wamepata fursa ya kumiliki nyumba zao bora na wananchi wengi wanaupongeza mpango huu wa Shirika na wao wenyewe wanasema kwao ni ukombozi mkubwa.
"Sera yetu ni kuwa bega kwa bega katika kutimiza malengo ya serikali. Iko hivi, tangu mwanzo kabisa NHC tumekuwa pamoja na serikali katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati.
Miradi hiyo ilitekelezwa na Shirika kama mkandarasi. Na katika kuunga mkono uamuzi wa serikali wa kuhamia Dodoma, shirika lilishiriki kujenga majengo ya ofisi za wizara nne eneo la Mtumba Dodoma uliko mji wa serikali." anasema Dk. Banyani na kuzitaja Wizara hizo kuwa ni ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Fedha na Mipango, Viwanda na Biashara na Wizara ya Nishati.
"Iyumbu Dodoma tumejenga takriban nyumba 300 kwa ajili ya makzi na zimeshauzwa kwa wananchi na taasisi za serikali. NHC tunakimbizana na serikali mgongoni katika kutekeleza kauli mbiu ya hapa kazi tu. Sisi NHC tunakimbia mchaka mchaka nchini.
Shirika katika kuondoa tatizo la makazi na ofisi za watumishi wa umma katika taasisi mbalimbali, limesanifu na kujenga majengo 44 ya Wakala wa Misitu Tanzania ili kuwapatia makazi na ofisi za kulinda misitu yetu." anasema Dk. Banyani.
Anasema, Shirika limekarabati shule kongwe mbalimbali nchini, chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na pia limeshiriki katika kujenga nyumba za wafanyakazi katika Halmashauri za Busokelo iliyoko mkoani Mbeya, Mlele mkoani Katavi, Momba mkoani Songwe, Muheza mkoani Tanga na Chato mkoani Geita.
Ili kufanya Halmashauri za Wilaya kuwa na majengo ya kisasa ya Ofisi na kuongeza tija, Shirika la Nyumba la Taifa limejenga majengo ya ofisi katika Halmashauri ya Malinyi na Halmashauri ya Wanging’ombe na pia Jengo la Utawala la Mkuu wa Wilaya ya Hai na Malinyi.
Dk. Banyani anataja miradi mingine iliyotekelezwa na NHC kwa ukandarasi katika kipindi hiki kuwa ni ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya EWURA Mjini Dodoma na ujenzi wa jengo la Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere mkoani Mara.
"Pia tumefanya ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Benki la CRDB, Jijini Dar es Salaam, Jengo la Chuo Kikuu cha Ardhi na ujenzi wa shule ya watoto wenye mahitaji maalum huko Mbuye Mkoani Geita.
Kupitia utaratibu huu, shirika liliaminiwa na serikali na kupewa kujenga miradi ya kimkakati ambayo itaongeza tija kubwa kwa Taifa letu.
Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa machinjio ya kisasa eneo la Vingunguti Jijini Dar es Salaam, ambayo itakuwa na uwezo wa kuchinja ngombe 1500 na mbuzi 1000 kwa siku, ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo Mtwara na Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kwangwa, Mjini Musoma.
Miradi yote hii inayofanywa na shirika kama mkandarasi iko 26 na ina gharama ya sh. bilioni 86.2 hadi kuikamilisha." anasema Dk. Banyani.
"Lakini pia shirika limeendelea kujenga uwezo wake kwa kukusanya kodi na malimbikizo kutoka kwa wapangaji wake na limepangisha nyumba zake zilizojengwa katika Halmashauri za Wilaya na Miji mbalimbali nchini.
Kwa sasa matengenezo ya nyumba yanazingatia uwiano wa gharama na matengenezo yenyewe ili kuokoa gharama za matengenezo na muda unaotumika katika kazi hii." Dk. Banyani na kuongeza;
"Kazi zinazoendelea kufanywa na shirika kwa sasa ni pamoja na kuanza usanifu na maandalizi ya ujenzi wa nyumba 1000 za makazi jijini Dodoma na tunaendelea na kazi ya ujenzi wa Ofisi ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Kanda ya Kati Dodoma.
Aidha, Shirika tumeanza kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya utengenezaji wa vifaa vya ujenzi kama vile kokoto, matofali na mabati. Hapa NHC tunatekeleza kwa vitendo
ile dhana ya Tanzania ya viwanda.
Katika utekelezaji wa dira ya serikali ya Awamu ya Tano, Shirika limelenga kuongeza ajira kwa watanzania, kuwapatia makazi bora na kuunga mkono serikali katika ujenzi wa miradiya kimkakati yenye kuboresha maisha ya Watanzania".
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇