LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 15, 2020

NGEMELA LUBINGA AWASILI MKOANI GEITA KWA ZIARA YA KIKAZI

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayeshughulika na Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akiwasili Geita

CCM Blog, Geita
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayeshughulika na Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga amewahakikishia viongozi wa Chama na Serikali mkoani Geita kwamba kwa jinsi CCM ilivyojipanga na kusimamia ilani yake vizuri, itashinda katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba Mwaka huu.

Amewataka viongozi hao kuhakikisha wanakuwa makini na kusimamia na kuzingatia taratibu zote ili kuhakikisha ushindi wa kishindo ambao CCM itaupata hauna doa, kwa kuwa CCM ndicho chama chenye dhamana ya kuongoza Serikali.

Kanali Mstaafu Ngemela aliyasema hayo, jana alipozungumza na viongozi wa Chama na Serikali, baada ya kuwasili mkoani Geita kufanya ziara ya kikazi.

‘’Tunataka kuwaletea wananchi maendeleo kama haya yanayoletwa na Chama Cha Mapinduzi waliyokuwa wakiyasubiri.’’ alisema Kanali Mstaafu Lubinga baada ya kusomewa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ulivyofanikiwa katika mkoa huo.

Kanali mstaafu Lubinga, ambaye pia ni Mlezi wa Mkoa wa Geita  baada ya kuwasili alipokewa na Viongozi wa Chama na Serikali na baadaye kukutana na Viongozi wa Kamati ya Siasa ya Mkoa na kupokea taarifa mbali mbali zinazohusiana na mkoa huo.

Pia Mkuu wa Mkoa Geita Mheshimiwa Injinia Robert Gabriel aliwasilisha taarifa ya miradi mbalimbali kama vile  ujenzi wa shule na zahanati kama Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages