Ripoti ya matukio ya Kiislamu inahusu mwongozo uliotolewa na Mufti wa Tanzanua Sheikh Abubakar Zubeir Ali leo Ijumaa kuhusiana na ugonjwa wa Corona ambapo amemshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuitikia Dua za watanzania.
Taarifa iliyosomwa na msemaji wa mufti Sheikh Hassan Chizenga, mufti ametoa muongozo huo kufuatia habari ya kupungua maambukizi ya Corona nchini Tanzania. Amesema kuwa, kutokana na maendeleo hayo, vyuo vya dini ya Kiislamu ambavyo vina watu wazima, wanafunzi warejee kama ilivyotangazwa na serikali. Ama watoto wadogo waendelee kusubiri mpaka serikali itakapotoa maelekezo mengine. Ama nukta nyingine ni kwamba, mikusanyiko ya kidini na kiibada nje ya nyumba za ibada kama vile kumbi na mfano wake zitakazowahusu watu wazima zitaendelea kwa kuzingatia taratibu za Afya zilizowekwa.
Na tukio lingine miongoni mwa matukio ya Kiislamu, ni mauaji yaliyofanywa kusini mwa pwani ya Kenya eneo la Diani ambapo baba mmoja na watoto wake wawili, waliuawa kinyama kwa madai kuwa eti walikuwa wanachama wa ash-Shabab. Kufuatia jinai hiyo, asasi zote za Kiislamu nchini Kenya zimeitaka serikali kuwachukulia hatua kali polisi wote waliohusika na unyama huo kwa kuwa watoto wadogo hawafai kuhusishwa na kosa wasilolijua.
Mwandishi wetu wa visiwani Zanzibar, Harith Subeit ana ripoti zaizi……../
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇