LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 2, 2020

MKUTANO MAALUM WA 41 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI TAREHE 4 – 5 JUNI, 2020





Mkutano Maalum wa 41 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki utafanyika tarehe 4 na 5 Juni 2020 kwa njia ya mtandao (Video Conference). Mkutano utafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara uliopo Mji wa Serikali, Mtumba – Dodoma.

Mkutano huo Maalum wa 41 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki, utaanza kwa mkutano wa ngazi ya wataalam tarehe 4 Juni, 2020 na kufuatiwa na mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu tarehe 5 Juni 2020 na kisha kufuatiwa na mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki siku hiyohiyo (kuanzia

saa 9:00 alasiri hadi saa 11:00 jioni).

Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo utajadili masuala ya fedha na utawala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages