LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 15, 2020

MAUAJI YA KIMBARI RWANDA: 'MIMI NI MAMA-NILIUWA WAZAZI WA BAADHI YA WATOTO'

Fortunate Mukankuranga


Haki miliki ya pichaNATALIA OJEWSKA

Maelfu ya wanawake walishiriki mauaji ya kimbari ya Rwanda 1994 lakini jukumu lao halijakuwa likizungumziwa, hali inayofanya maridhiano na familia zao kuwa ngumu.
Mwanahabari Natalia Ojewska amekuwa akizungumza na baadhi ya wanawake hao gerezani.
Kitu kilichoanza kama shughuli ya kawaida ya wanawake kuenda mtoni kuteka maji ya kutayarisha kiamsha kinywa, kiliishia kumfanya Fortunate Mukankuranga kutekeleza mauaji.
Akiwa amevalia sare za wafungwa huku akiongea kwa sauti ya upole, alikumbuka matukio ya asubuhi ya Jumapili, Aprili 10,1994.
Alikuwa njiani, alipokutana na kundi la washambuliaji likiwapiga wanaume wawili katikati ya barabara.
"Wakati [wawili hao] walipoanguka chini, Niliinua kijiti na kusema: 'Watutsis lazima wafe!'. Kisha nikampiga mmoja na kufuatilia na wa pili… Nilikuwa mmoja wa wauaji," alisema mama huyo mwenye umri wa miaka 70.

Kujitia mauaji

Wanaume hao wawili ni miongoni mwa watu 800,000 kutoka kabila la Tutsi na Wahutu wenye misimamo ya kadiri waliouawa kwa zaidi ya siku 100.
Baada ya kutekeleza mauaji, Mukankuranga, ambaye ni Mhutu, alirejea nyumbani kwa watoto wake saba akiwa na fedheha akikumbuka alichofanya.
"Mimi ni mama. Niliua wazazi wa baadhi ya watoto," alisema.
Siku chache baadae, watoto wawili wa Kitutsi waliokuwa wamejawa na uoga baada ya wazazi wao kuuawa kwa kukatwa mapanga, walibisha mlango wake kuomba hifadhi.

Aibu ya kuwa mkosa'

Hakuchelea kuwasaidia watoto hao ambao hatimaye waliponea mauaji lakini alijutia hatua yake ya awali.
"Licha ya kwamba niliwapatia hifadhi watoto, Nilihisi nimewakosea wanaume hao wawili. Usaidizi huo hautawahi kuondoa aibu ya kuwa mkosa," anasema Mukankuranga.
Yeye ni mmoja wa wanawawe wanaokadiriwa kuwa 96,000 ambao wamefungwa kwa kuhusika katika mauaji ya kimbari - baadhi yaoa kama vile Mukankuranga, waliwaua watu wazima, wengine waliwaua watoto, na wengine wakiwaua wazee na kuwashawishi wanaume kubaka na na kutekeleza mauaji.
Usiku wa tarehe 6 Aprili 1994, ndege iliyokuwa imembeba Rais wa Rwanda Mhutu Juvenal Habyarimana ilidunguliwa lipokuwa anakaribia kutua katika uwanja wa ndege mjini, Kigali.
Japo waliotekeleza mauaji hayo hakuwahi kujulikana, Wahutu wenye misimamo mikali moja kwa moja waliwalaumu waasi wa kutoka kabila la Watutsi kwa walitekeleza shambulio hilo.
Ndani ya saa kadhaa, maelfu ya Wahutu ambao wamekuwa na uhasama wa miongo kadhaa ya chuki za kabila, walianza kueneza propaaganda na kuanza kutekeleza mauaji yaliyopangwa.
Ushiriki wa wanawake katika mauaji hayo yalienda kinyume na dhana ya kwamba wao ni walinzi wa familia na sauti ya busara.
"Ni vigumu kuelewa jinsi mwanamke anayependa watoto wake, anaweza kuenda kwa jirani' [nyumbani] kuua watoto wao," anasema Regine Abanyuze, mfanyakazi wa shirika lisilo la kiserikali la Never Again, ambalo linajishughulisha na masuala kuleta ya amani na maridhiano.
Ghasia zilipozuka nchini, maelfu ya wanawake waligeuka kuwa maajenti wa vurugu kwa kushirikiana na wanaume.

Women sewing in a groupHaki miliki ya pichaNATALIA OJEWSKA
Image captionMagerezani wanawake walipewa muda wa kukiri makosa yao

Pauline Nyiramasuhuko, alikuwa waziri wa zamani wa familia na maendeleo ya wanawake , ni miongoni mwa wanawake walichukua nafasi za juu ambazo wengi walikuwa wanaume nchini Rwanda.

Mitazamo miwili ya mauaji

Martha Mukamushinzimana ni mama wa watoto wa tano, ambaye amekuwa akibeba siri nzito kwa miaka 15 ya uhalifu, kabla hajaamua kujiripoti mwenyewe katika mamlaka za sheria mwaka 2009 wakati ambao alikuwa anashindwa kuendelea kujizuia kukaa na siri ya uhalifu alioufanya.

Martha MukamushinzimanaHaki miliki ya pichaNATALIA OJEWSKA
Image captionMartha Mukamushinzimana anasema alikuwa anafuata maelekezo tu

Katika kujitathimini wenyewe katika jukumu la uzazi kama mama, wengi huzidiwa sana na aibu kukubali kwa wapendwa wao kwamba walishindwa katika jukumu lao kama walezi.
"Katika kipindi hiki tunatumia chombo maalumu cha kujirekebisha. Tunataka kuwapa muda wa kutosha na muhimu kuwasikiliza na taratibu kuwafanya wakiri makosa yao, ," alisema Grace Ndawanyi, mkurugenzi wa gereza la wanawake huko Ngoma, jimbo la mashariki mwa Rwanda.
"Kwa sababu nyumba yangu ipo karibu na barabara, Nilikuwa nasikia hekaheka zote na kuona jirani zangu watutsi wakiwa wanafungwa na kupelekwa kanisani," alisema Mukamushinzimana, akiwa amekaa katika sehemu ndogo ya wazi katika chumba cha gereza, na ,mara nyingine akiwa analia.
Maelfu ya watutsi, walifanyiwa uhalifu ndani au katika maeneo ya parokia ya Nyamasheke , walikuwa wanapambania maisha yao kwa wiki.
Stanislus Kayitera, sasa ana miaka 53, alikuwa miongoni mwa watu walionusurika . Ana kovu kubwa la jeraha ambalo alipata kutokana na bomu .
"Ninakumbuka wanawake wakiwa wanakusanya mawe na kuwapa wanaume, ambao walikuwa wanatupiga nayo.Walikuwa wanapiga risasi na kurusha mabomu na kunyunyizia mafuta kwa watu na kuwasha moto.
"Na walikuwa wanashambulia makanisa na kuanza kutuua kwa kwa makundi,"alisema bwana Kayitera, ambaye alinusurika kwa sababu alikuwa amejificha chini ya mwili wa marehemu.
Mukamushinzimana anasema alikuwa analazimishwa kufuata amri.
"Nilimbeba mwanangu mgongoni na kuungana na kundi la wanawake waliokuwa wanakusanya mawe kwa ajili ya kuua watu waliokuwa wanajificha kanisani," alisema Mukamushinzimana, ambaye alikuwa amejifungua siku mbili kabla.
Wakati alipoingia gerezani mwaka 2009, hakuna ndugu yake hata mmoja aliyekuwa tayari kumsaidia kuangalia watoto wake watano.

A woman in prison sewingHaki miliki ya pichaNATALIA OJEWSKA

"Mauaji ya kimbari yalikuwa mapambano dhidi ya jamii yote. Mapigano hayo yaliathiri utu wa watu waliofanyiwa ubaya lakini pia wahusika wenyewe. Na hao watu wanahitaji kupona kutoka katika changamoto hiyo pia," alisema Fidele Ndayisaba, katibu mkuu wa kamati ya maridhiano kitaifa ya Rwanda.
Wanawake waliohusika na mauaji ya kimbari wanasisitizwa kuandika barua kwa familia zao na ndugu za watu waliowafanyia ubaya ili kupata ukweli hatua kwa hatua na kuweza kusameheana.

Presentational grey line


Presentational grey line

Wakati wanapotoka gerezani, wanawake waliohusika katika mauaji ya kimbari huwa wanakutana na wakati mgumu sana ukilinganisha na wanaume.
Baadhi wanakuta waume zao wameoa na kuwatoa katika urithi wa mali zao.
Jamii zao nyumbani hawataki kuwakaribisha na wanakuwa wanaangaika na kukataliwa na ndugu zao wa karibu.
Lakini kuna jitihada kubwa ambayo inachukua muda mrefu na bado baadhi ya wafungwa ambao wanakuwa wanasita kukataa itikadi za chuki za kikabila.
"Ni kweli tuna baadhi ya watu ambao wanakataa kukubali makosa yao. Kuna ambao ni wagumu lakini idadi yao inapungua," alisema bwana Ndayisaba.
'Sikuweza kujizuia machozi'
Fortunate Mukankuranga alipata nguvu ya kukiri uhalifu aliofanya miaka minne baada ya kufungwa mwaka 2007.
Anakumbuka kuwa alikuwa anajisikia hofu kabla hajaomba msamaha mtoto wa mmoja wa kiume wa miongoni mwa watu aliowauwa.
Bila kutegemea "alikuwa amefurahi wakati alipokutana naye na alitokwa machozi na alimkumbati," alisema.
Kwa sasa Mukankuranga anaangalia jinsi siku za mbeleni zitakavyokuwa, ana matumaini kuwa atarudisha uhusiano mzuri na wapendwa wake.
"Nikirudi nyumbani, nitaishi kwa amani na familia yangu na nitakuwa na utu wa kuwapenda wengine zaidi na kuwajali. Ninalipa sasa uhalifu niliofanya. Sikupaswa kuwa gerezani mimi kama mama," aliongeza.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages