LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 7, 2020

HARAMBEE KUCHANGIA MIUNDOMBINIU YA SHULE YA MSINGI KASHATO MKOANI KATAVI YAFANA

Na Aidan Felson,
Mpanda-Katavi.

Harambee ya kuchangia maendeleo ya miundombinu kwa Shule ya Msingi Kashato iliyopo Kata ya Makanyagio Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imeanza na tayari Diwani wa Kata hiyo Mhe. Haidari Sumri ameanza kwa vitendo kuonesha njia.

Kwa kutambua umuhimu wa elimu, Diwani Sumri amekabidhi mchango wake wa matofali 3,000 yenye thamani ya Shilingi Milioni 4 ili kuongeza miundombinu katika Shule hiyo iliyoanzishwa Mwaka 1963.

Shule ya Kashato inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya Madarasa 26 kati ya madara 9 yaliyopo ambayo yanawahudumia Wanafunzi 1,323.

Akikabidhi mcahngo wake katika hafla aliyoiandaa katika viunga vya Shule hiyo pamoja na michango mingine Mhe. Sumri amewataka viongozi wanaobaki wakati yeye akimaliza muda wake wa udiwani,wahakikishe michango inafanya kazi iliyokusudiwa, huku akiwashukuru Wadau waliojitokeza kumuunga mkono kwenye harambee hiyo.

Katika hafla hiyo, ambayo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mh Lilian Charles Matinga, Mkurugenzi wa Manispaa ya Wilaya ya Mpanda Ndugu Michael Nzyungu amempongeza Mh Sumri kwa kitendo hicho cha kizalendo

Ndugu Nzyungu amesema michango ya namna hiyo inaifanya Serikali ipunguziwe mzigo wa kuwatoza ushuru wafanyabiashara wadogo wadogo kwa kuwa baadhi ya mahitaji yanachangiwa na Wadau.

Kwa upande wake mgeni rasmi ameitaka jamii kuwa na tabia ya kumsifia mtu akiwa hai pale anapofanya jambo zuri, huku akiwahimiza wadau wengine kuendelea kujitolea kwa kuwa mchango huo unakwenda kuwasaidia watoto wao na watoto wa wengine. 

Katika harambee hiyo kiashi cha shilingi  Milioni 7,140,000/= zimepatikana kutoka kwa kadau mbalimbali, kati ya hizo pesa taslimu zikiwa Shilingi Milioni 2,440,000/= huku fedha pamoja na vitu vilovyoahidiwa ni shilingi milioni 4,700,000/=.Vile vile imechangwa mifuko ya saruji 205,Kokoto tripu 1 na Mchanga tripu 13.

Muonekano wa sehemu ya Shule ya Msingi Kashato iliyopo Kata ya Makanyagio Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi  
Sehemu ya matofali yaliyochangwa kwenye bharambee hiyo
Diwani Haidari Sumri akiongea kwenye harambee hiyo


Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Lilian Charles Matinga akiongea kwenye harambee hiyo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages