LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 23, 2020

CCM YAWAONYA WATIA NIA WANAOCHAFUA MADIWANI NA WABUNGE WANAOMALIZA MUDA WAO

Mbunge wa viti Maalumu CCM Mkoa wa Kagera akizungumza na viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kutoka Kata zote za Manispaa ya Bukoba jana mjini Bukoba.(Picha na Allawi Kaboyo).

Na Allawi Kaboyo, Bukoba
Wenye nia za kugombea Udiwani, Ubunge  katika Kata na Majimbo mkoani Kagera kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameonywa kuacha tabia ya kutoa kauli za kuwachafua madiwani na wabunge wanaomaliza muda wao kama njia rahisi ya kushinda nafasi hizo katika Uchaguzi Mkuu uliopamgwa kufanyika Oktoba Mwaka huu wa 2020.

Akizungumza mjini Bukoba juni 22, mwaka huu na viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) kutoka kata zote za Manispaa ya Bukoba, Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Kagera Bernadeta Mushashu amesema kumekuwepo na tabia ya baadhi ya Wana CCM watangaza nia wanaowachafua madiwani na wabunge wanaomaliza muda wao wakitaka kuchukua nafasi zao.

Mushashu ameleza kuwa amekuwa akipokea tuhuma nyingi kutoka kwa madiwani wa mkoa huo kuwa wanachafuliwa kwa kashifa nzito kutoka kwa wanachama wanaotaka kutangaza nia akiwemo yeye ambapo amewatahadharisha wale wote wenye tabia hiyo waache mara moja kwa kuwa chama chake bado kinawatambua kama viongozi.

“Nimesikitishwa na wanaccm wenzetu wanaotangaza nia za kugombea nafasi mbalimbali hapa mkoani mwetu kuanza kutuchafua na kututolea maneno ya kashifa kwa wananchi kisa uongozi hili sio jambo la kiungwana ndugu zangu, mimi mwenyewe nimeshasemwa mengi likiwemo hili la mimi kuwa mremavu wapo wanaosema kuwa sistahili kuwa mbunge kisa mimi ni mremavu wa miguu kuwa nikagombee viti maalumu vya walemavu kiukweli suala hili limeniuma sana.” Alieleza Mbunge Mushashu

Ameongeza kuwa wanaotaka nafasi za uongozi wala hawazuiliwi lakini wasiwachafue viongozi wanaomaliza muda wao kwa kuwasema vibaya na kuwapa tuhuma ambazo sio zao huku akifafanua kuwa wabunge na madiwani bado wananendelea na majukumu yao hadi hapo tarehe za kuchukua form za kugombea zitakapo timia na watauacha ubunge na udiwani pindi wabunge na madiwani wapya watakapoaapishwa.

Mbunge huyo ameleza mambo makubwa ambayo ameyafanya katika kipindi cha miaka mitano tangu achaguliwe kama mbunge viti maalumu ambapo kwamba katika kipindi hicho ametumia zaidi ya sh. Bilioni 11.7 katika masuala ya maendeleo ikiwemo kuchangia baadhi ya michango kuanzia ngazi ya kitaifa hadi ngazi ya kijamii pamoja na Sacco’s mbalimbali mkoani Kagera.

 Kwaupande wake Katibu Mwenezi wa mkoa huo Hamimu Mahamudu amesema kuwa CCM inawategemea kinamama katika kuhakikisha wanashinda uchaguzi mkuu ujao kwa mshikamano wao huku akiwasihi kuacha kupigana majungu na badala yake wanatakiwa kuwa wamoja.

Hamimu amesema kuwa katika kipindi ambacho wanawake wamependelewa na kupewa nafasi za uongozi basi ni kipindi cha serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dk John Magufuli hivyo wanaowajibu wa kuhakikisha chama chao kinashinda kwa wagombea wao kupata kura za kutosha, ambapo pia ametumia nafasi hiyo kuwaomba kinamama hao kuhakikisha kata zote za manispaa ya Bukoba zilizokwenda upinzani zinarudi CCM pamoja na jimbo.

“Sisi kama chama tunatambua kuwa wanawake ni jeshi kubwa tena jeshi la ushindi, hivyo niwaombe wakina mama mkibebe chama hiki na kuhakikisha kinapata dola, katika mkoa wa Kagera Bukoba mjini ndiyo halmashauri pekee pamoja na jimbo ambavyo vimekwenda upinzani hivyo mnao wajibu wa kuhakikisha vyote vinarudi.” Ameeleza Mahamudu.

Mahamudu amewakemea watia nia wanaopita na kuomba nafasi kabla ya muda huku wakitoa kashifa na majungu kwa wabunge na madiwani wanaomaliza muda wao kwa kusema hali hiyo haikubaliki nawote watachukuliwa hatua.

Amewataka wagombea wagombee kwa utaratibu uliowekwa na chama chao na kuwasihi wagombea na wana CCM kwa ujumla kujiepusha na vitendo vya rushwa katika kipindi chote cha uchaguzi na kusema kuwa CCM haitawaacha salama wote watakaobainika
Mbunge wa Viti Maalumu wa CCM Mkoa wa Kagera (kulia) akimkabidhi Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa huo Hamimu Mahamudu Sh.Milioni 2 alizoahidi wakati wa uzinduzi wa Kagera ya Kijani kwa ajili wa ukarabati wa ofisi ya CCM Mkoa huo.(Picha na Allawi Kaboyo).

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages