LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 24, 2020

WAPALESTINA WASHAMBULIWA KATIKA SWALA YA EID EL FITRI

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, wanajeshi wa utawala ghasibu siku ya Jumapili  asubuhi waliwashambulia  Wapalestina waliokuwa wamefika kando kando ya msikiti wa Al Aqsa kwa ajili ya Swala ya siku kuu ya Eid el Fitri.
Pamoja na kuwepo utumiaji mabavu wa askari wa Kizayuni, Wapalestina hao hatimaye waliweza kuswali Swala siku kuu ya Eid el Fitri katika Medani ya Al Ghazala katika uwanja wa Msikiti wa Al Aqsa katika lango la Babul Asbaat la msikiti huo.
Msikiti wa Al Aqsa
Eneo la ndani la Msikiti wa Al Aqsa limefungwa kwa muda wa miezi miwili sasa kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 na kwa mujibu wa Idara ya Wakfu ya Palestina, msikiti huo utafunguliwa kikamilifu baada ya siku kuu ya Eid el Fitri.
Leo Jumapili, tarehe Mosi Shawwal ni siku kuu ya Idul Fitr katika aghalabu ya nchi za dunia. 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages