CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema)kimetajwa kukosa ajenda ya kisiasa na badala yake kimeamua kutumia ajenda ya janga la Corona linalosababisha homa kali ya mapafu(Covid 19)lililopo nchini kama mtaji wao wa kisiasa.
Kutokana na hilo kimetakiwa kujiandaa kushindwa kwa asilimia kubwa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwak ufanyika mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Mei 22 jijini Dodoma mbunge wa Ukonga Mwita Waitara amesema chama hicho kilitaka kutumia janga la Corona kama mtaji wao wa kisiasa kwa kutaka nchi iwafungie watu wake ndani na wasitoke nje.
“Walitaka kuwe na lockdown ili baadae uchaguzi usogezwe mbele na wao waendelee kuwepo katika nafasi zao lakini nashukuru Rais wetu Dkt John Magufuli alielewa lengo lao mapema hakuruhusu hilo litokee,alisema uchaguzi upo pale pale, ukifanya lockdown ya nchi hatuna uwezo wa kusupply chakula kwa watu hivyo wangefanya uporoji au kufa kwa njaa na wao wangesema watu wapewe chakula,ingeshindikana wangepiga kelele na kupata mtaji wa kisiasa,”alisema Waitara.
Waitara ambaye pia ni Naibu Waziri,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa(Tamisemi) amesema chama hicho kupitia mwenyekiti wake Freeman Mbowe kimekuwa kikifanya ubadhirifu wa fedha huku kikiwanyanyasa baadhi ya wabunge ambao wamejitolea kuwasemea wananchi kwak uhudhuria vikao vya bunge na kuacha kufuata maelekezo ya kukaa karantini kama walivyoamuriwa hapo awali.
Amesema Chadema pamoja na kupata shilingi bilioni 23.58 kupitia makusanyo ya wabunge wake kwa kipindi cha miaka mitano, bado jengo la makao makuu ya chama hicho wamepanga.
“Mwaka 2014/2015 Mbowe alileta kampuni kutoka Marekani akasema hawa watafanya utafiti wa kufanya fund raising ya kupata fedha za kutosha ili Chadema ifanyie kampeni,na kampuni hii ililipwa sh milioni 500,sasa aje mtu wa Chadema atuambie hizo sh milioni 500 zilizolipwa wali raise kiasi gani na ziliingia kwenye akaunti gani na zilimsaidia mgombea gani,utaona hakuna majibu,
“Chama hiki kina vyanzo mbalimbali vya kupata Fedha,chanzo cha kwanza ni ruzuku ya Chadema wanalipwa milioni 326 ukipiga kwa miezi 60 utapata bilioni 19.56,chanzo Cha pili wabunge viti maalum wapo 36 wakilipa wote milioni 1.5 kila mwezi kwa miezi 60 unapata sh bilioni 3.2,chanzo cha wabunge tatu wabunge wa majimbo wapo 26 kila mmoja analipa laki 520 ukizidisha kwa miezi 60 unapata zaidi ya milioni mia 780,jumla ya fedha zote ni sh bilioni 23.58 ndio makusanyo ya miaka mitano ya chama hicho,lakini mpaka leo makao makuu kipande wamepanga kingine ndio wamenunua,”alisema Waitara.
Amewataka watanzania kujua aina ya chama hicho ambacho kinataka kuongoza nchi namna kinavyofanya ubadhirifu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇