LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 6, 2020

UMOJA WA AFRIKA KUCHUNGUZA DAWA YA CORONA YA MADAGASCAR


Umoja wa Afrika (AU) unafanya mazungumzo na Jamuhuri ya Madagascar, ili kupata data za kiufundi kuhusu usalama na ufanisi wa dawa ya mitishamba iliyotangazwa hivi karibuni ambayo ilidai inazuwia na kutibu Covi-19.

AU imesema kuwa Kamishna wa tume ya Umoja wa Afrika inayohusika na masuala ya kijamii Amira ElFadil alifanya mazungumzo na balozi wa Madagascar nchini Ethiopia Eric Randrianantoandro tarehe 30 April na wameafikiana kuwa nchi wanachama wataupatia maelezo muhimu Muungano wa Afrika kuhusu dawa za mitishamba.

Baada ya kupata maelezo Umoja wa huo kupitia kituo chake cha udhibiti wa magonjwa - (Africa CDC), kitatathimini data zilizokusanywa kuhusu usalama na ufanisi katika tiba hizo asili dhidi ya virusi vya corona.

Dawa hiyo inayohusishwa na mmea wa Kichina unaoitwa Artemisia (pakanga) - ambao ni mojawapo ya miti ambayo huchanganywa pamoja na mimea mingine ya Madagascar kama tiba ya ugonjwa wa Malaria.
 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages