LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 5, 2020

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO


Timo WernerHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWerner, katikati , aliwahi kufunga bao mwaka huu (2020) kwa penalti dhidi ya Tottenham
Liverpool wamewaambia wawakilishi wa Timo Warner,24, kuwa wanahitaji muda zaidi ili kuamua kama watatuma ofa kwa mshambuliaji huyo wa RB Leipzig, katika kipindi hiki ambacho wanasubiri kutathmini athari za ugonjwa wa corona katika dirisha la usajili. (Guardian)
Real pia wanaangalia uwezekano wa kumsajili kinda wa Rennes ya Ufaransa, Eduardo Camavinga, 17, ambaye Man United wanamwinda pia. (AS - in Spanish)
Paul PogbaHaki miliki ya pichaREX FEATURES
Image captionPaul Pogba alikuwa kama mchezaji wa akiba katika mechi dhidi ya Watford na Newcastle aliporejea baada ya kuuguza jeraha kwa miezi mitatu
Real Madrid wanajipanga kutuma ofa ya kumsajili mkiungo wa Man United na Ufaransa, Paul Pogba, 27. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Kiungo wa Sao Paulo ya Brazil Igor Gomez ,21, pia anawindwa na Real Madrid, lakini klabu yake haijapokea ofa rasmi. Vilabu vya Barcelona, Sevilla na Ajax pia vinaripotiwa kummezea mate. a(Goal via Globo Esporte)
Kiungo wa Atletico Madrid Thomas Partey, 26, ameweka wazi kuwa angelipendelea kuhamia katika klabu ya Arsenal na anaamini makubaliano ambayo yatamhusisha mshambuliaji Alexandre Lacazette kuhamia Atletico yatafanikiwa. (Telegraph)
Mesut Ozil prays before Arsenal's game against Manchester CityHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMesut Ozil, ambaye ni Muislamu, akisali kabla ya mechi ya Arsenal dhidi ya Manchester City
Klabu ya Uturuki ya Fenerbahce inaripotiwa kuwa katika mipango ya kumsajili kiungo wa Arsenal Mesut Ozil, 31, kabla ya mkataba wake kwisha mwakani. (Sun)
Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 28, yungali anataka kuihama PSG na kurejea Barcelona na inaaminika kuwa yupo tayari kukatwa mshahara kwa silimia 50 ili kutimiza azma yake ya kurudi Uhispania.. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Newcastle itawalazimu kuilipa Tottenham pauni milioni 12.5 kama watataka kumsajili kocha Mauricio Pochettino mwezi huu, lakini hawatatoa hata senti moja wakimchukua baada ya Mei 31. (ESPN)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages