LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 21, 2020

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO ALHAMIS 21.05.2020


Leroy SaneHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionLeroy Sane
Mshambuliaji wa Manchaster City, mjerumani Leroy Sane, 24, ametengewa jezi nambari 10 katika kikosi cha Bayern Munich kwa ajili ya msimu ujao. (Mirror)
Chelsea wanapambana kumuuza Victor Moses wakati Inter Milan wakikataa kulipa kitita cha pauni milioni 10.75, kwa jailli ya winga huyo wa Nigeria , 29.(Sun)
Wakala wa Jorginho, 28, amesisitiza kuwa kiungo wa Italia ana furaha katika kikosi cha Chelsea na kuda kuwa Juventus haijaonesha nia ya kumchukua mchezaji huyo. (Metro)
JorginhoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJorginho
Mlinda mlango wa Trabzonspors, na anayelengwa na Leicester City mturuki Ugurcan Cakir, 24 ametengewa kiasi cha euro milioni 20 na klabu ya Sevilla. (Leicestershire live)
Liverpool wako tayari kuwauza wachezaji watatu msimu huu ili kuweza kugharamia uhamisho wa pauni milioni 52 kwa ajili ya mshambuliaji wa miaka 24 wa RB Leipzig, mjerumani Timo Werner. (Athletic)
Timo WarnerHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTimo Warner
Manchester United wangependa kumshikilia mshambuliaji, 30, Odion Ighalo,kwa mkopo kutoka Shanghai Shenhua, lakini ''wamerudi nyuma'' kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo raia wa Nigeria baada ya Marcus Rashford afya yake kuimarika. (Sky Sports)
Arsenal wanafikiria kubadilishana wachezaji na Atletico Madrid kwa mshambuliaji wa kifaransa Alexandre Lacazette ,28 kwenda Uhispania, na Thomas Lemar, 24 kwenda Uingereza. (AS-in Spanish)
NeymarHaki miliki ya pichaUEFA /GETTY
Image captionNeymar
Neymar, 28, hataondoka Paris St-Germain kujiunga tena na Barcelona msimu huu kwasababu ya athari za virusi vya corona kwa uchumi wa vilabu vya mpira, ameeleza wakala wa mbrazili huyo. (Star)
Mizunguko ya awali ya Kombe la Carabao iko kwenye tishio ikiwa msimu ujao haitaanza kabla ya mwanzoni mwa mwezi Septemba. (Telegraph)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages