LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 19, 2020

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 19.05.2020

Gonzalo Higuain


Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionGonzalo Higuain

Juventus wanaweza kuuza wachezaji kadhaa akiwemo kiungo wa Bosnia Miralem Pjanic, 30 na mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain, 32, msimu huu kama sehemu ya sera mpya ya kifedha ili kuisaidia klabu kukabiliana na atahri za kiuchumi zilizosababishwa na janga la corona. (Daily Mail)
Kiungo wa Bayer Leverkusen Kai Havertz anapaswa kukataa nafasi ya kwenda Liverpool na badala yake ajiunge na Borussia Dortmund, anashauri mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani Jens Nowotny. (Goal)
Barcelona wanatarajia kuongeza juhudi katika kuhakikisha wanamsajili mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 22. (Mundo Deportivo-in Spanish)

Kalidou KoulibalyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKalidou Koulibaly

Manchester United wako tayari kurejesha tena nia yao ya kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa klabu ya Napoli, msenegali Kalidou Koulibaly, 28 baada ya kubaini kuwa Liverpool inamtupia macho nyota huyo. (Gazzetta dello Sport via Daily Express)
Mlinda mlango wa Liverpool Loris Karius, 26, hatarejea kufanya mazoezi na klabu hiyo kwa muda.Raia huyo wa Ujerumani amesitisha mkataba wake na klabu yake ya mkopo Besiktas mapema mwezi huu. (Daily Star)

Loris KariusHaki miliki ya pichaANP SPORT/GETTY
Image captionLoris Karius

Winga anayechezea Newcastle kwa mkopo,Valentino Lazaro anasubiri kusikia kutoka mwa Mkurugenzi Mtendaji Lee Charnlet kuhusu mustakabali wake msimu ujao.
Mchezaji huyo, 24 alijiunga na Magpies akitokea Inter Milan mwezi Janurari. (Newcastle Chronicle)
Manchester City wana imani kuwa David Silva, 34 atakubali kuingia mkataba wa muda mfupi ili kumsaidia kiungo huyo wa kati kumalizia msimu huu. Kiungo huyo raia wa Uhispania anatarajiwa kuondoka mwezi Juni mkataba wake utakapomalizika. (ESPN)

David SilvaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDavid Silva

Manchester United wanajiandaa kumuita mlinda mlango wa Ureno Joel Pereira anayecheza kwa mkopo katika klabu ya Hearts baada ya kuhitimisha msimu wa ligi kuu ya Uskochi. (Manchester Evening News)
Wolves wameongeza mkataba wa mlinda mlango wa kiingereza John Ruddy,33, kwa mwaka mmoja zaidi. (Birmingham Mail)

David SilvaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDavid Silva

Kocha wa Chelsea Frank Lampard ana matumaini kuwa wachezaji wake waliomaliza mkataba watasaini mkataba wa muda mfupi, kuongeza kwenye mikataba yao, ambayo inatarajiwa kuisha kabla ya mwisho wa msimu huu. Mikataba ya kiungo Willian, 31 na mshambuliaji Olivier Giroud,33, inatatarajiwa kumalizika tarehe 30 mwezi Juni.(Chelsea)
Mshambuliaji wa kiingereza wa klabu ya Watford Troy Deeney ana hofu wachezaji wa ligi ya primia watapata upinzani kuhusu vipimo vya virusi vya corona.(Goodmoring Britain via Evening Standard)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages