LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 26, 2020

STOP KUTUMIA NAMBA YA TAHADHARI YA MAJANGA YA MOTO KWA KUTOA TAARIFA ZA UONGO

Na Lydia Lugakila
KAGERA

 Wananchi Mkoani Kagera wametakiwa kuacha mara moja tabia ya  kutoa taarifa zisizo za kweli kwa kutumia namba ya tahadhali inayotumika kutoa taarifa kwa jeshi la zimamoto na uokoaji.

kauli hiyo imetolewa  na mkaguzi wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Kagera Thomas Majuto wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ambapo amesema kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa wakitumia vibaya namba ya tahadhali inatumika kutoa taarifa za majanga yakiwemo ya  moto.

Aidha katika hatua nyingine Majuto amewahimiza watumiaji wa gesi kuhakikisha wanajenga uratibu wa kukagua mapaipu ya majiko ya gesi ili kuepuka majanga ya moto.

Hata hivyo Mkaguzi huyo ametoa wito kwa madreva wa vyombo vya moto kuacha tabia ya kupakia mafuta katika  vituo vya mafuta wakiwa  wamebeba abiria katika vyombo vyao  vya  moto jambo ambalo ni hatari .

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages