LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 27, 2020

RAIS MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI, CHAMWINO, DODOMA

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Mawaziri Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mawaziri pamoja na Manaibu Mawaziri leo tarehe 27 Mei 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama kwa dakika moja pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mawaziri pamoja na Manaibu Mawaziri ili kumkumbuka na kumuombea aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Marehemu Balozi Augustine Mahiga kabla ya kuanza kwa Kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages