LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 14, 2020

PROF. KABUDI ATAJA SABABU ZA TANZANIA KUTOSHIRIKI MKUTANO WA NCHI NNE NA ULE ULIOTISHWA NA RAIS WA AFRIKA KUSINI



Na Said Mwishehe, Michuzi TV.

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amefafanua kwa kina sababu za Tanzania kutoshiriki kwenye mikutano ya kikanda ukiwemo mkutano wa Korido ya Kaskazini unaohusisha nchi nne pamoja na mkutano wa SACU uliotishwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.

Ufafanuzi wa Profesa Kabudi ambao ameutoa leo Mei 13,2020 Bungeni Mjini Dodoma unatokana na kuwepo kwa madai ya baadhi ya watu wasioitakia mema Jumuiya Afrika Mashariki kuzusha maneno yasiyo ya kweli kuhusu jumuiya hiyo.

Akizungumza zaidi Bungeni, Profesa Kabudi ameanza kwa kuelezea mkutano uliohusisha nchi nne ambazo zinaunda Korido ya Kaskazini(Ushoroba wa Kaskazini) ambapo amesisitiza mkutano huo haukuwa unaihusu Tanzania ingawa ilikuwa na taarifa za kufanyika kwake.

"Mkutano ambao umefanyika ni wa Korido ya Kaskazini na walitutaarifu na tulijua, kwanini walitutaarifu lakini kwanini tuhudhurie mkutano wa Korido ya kaskazini? Ni wa kwao , ule haukuwa mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

"Na sitaki kurudia aliyoyasema Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2012, hayo yamepita tusiruhusu maadui zetu kutaka kuitingisha Jumuiya hii ya Afrika Mashariki. Wana yao na sisi tusiwe sehemu ya hayo, ndwele si sifa lakini Tanzania haijawahi kuacha kusimamia maslahi yake pamoja na udogo wa nchi hii kiuchumi.

"Nchi hii(Tanzania) imefanya mambo makubwa sana kwa hiyo nataka kuwahakikishia mkutano ule wa zile nchi nne ulikuwa ni mkutano wa majadiliano wa Korido ya kaskanini,lakini sisi na rwanda tumekuwa na centre Corido , ndio maana sisi na Burundi hatukwenda, kwasababu Burundi ni Centre Corido.Kwanza utafanyikaje bila sisi kualikwa.kwanza nilitaka hilo lieleweke na watu wasikuze,"amesema Profesa Kabudi wakati anatoa ufafanuzi.

Ameongeza tumshukuru Rais mstaafu Jakaya Kiktwete mwaka 2013 alipolisemea hilo na hali imebadilika. Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda alinitaarifu kuhusu mkutano huo na kwamba ni wa kwao na umeendelea.
Kuhusu mkutano ulioitishwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Profesa Kabudi amesema kuwa Rais huyo haikutisha mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC),kwani mkutani wa SADC inatishwa na Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo kwa kushiriana na Mwenyekiti ."Hiyo ni mikutano ya SADC."

Amesema kuwa mkutano uliotishwa na Rais Ramaphosa ulikuwa ni mkutano wa nchi ambazo ni majirani wa Afrika Kusini(SACU)ambao wengi wao wako SACU ukiondoa Zimbabwe ingawa inapakaa na Afrika kusini, Msumbuji na Angola na ndio maana nchi nane hazikuhudhururia.

Profesa Kabudi amezitaja nchi ambazo hazikuhudhuria mkutano huo wa SACU ni Tanzania, Zambia, Malawi,Madagasca, Mauritius, Comoro na DRC na ili kolamu ya vikao vya SADC itimie kunapaswa kuwa na watu 11.

"Na waliomsikiliza Rais Ramaphosa alisema mkutano SADC haukuitishwa kwa sababu ya lojistiki , ndio kwasababu anayeitisha vikao vya SADC ni Katibu Mtendaji wa SADC na ambaye kwa sasa ni Dk.Stergomena Tax na ukweli ni kwamba katika nchi zote hizo tuna mahusiano mazuri,"amesema Profesa Kabudi.
Mwisho

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages