LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 26, 2020

MJI WA SERIKALI DODOMA UTAKAPOKMILIKA UTAGHARIMU ZAIDI YA TRILIONI 10


Eneo: Jiji la Dodoma imetenga eneo la mji wa Serikali ambao upo katika Kata ya Ihumwa kilomita 17 kutoka katikati ya Mji. Eneo hili lina ukubwa wa Hekta 617.15 sawa na Ekari 1,542.88.
Mipaka: Mji wa Serikali kwa upande wa  mangaribi unapakana na kambi ya Jeshi ya Ihumwa, Kaskazini-Mashariki unapakana na kata ya Mtumba na upande wa Kusini unapakana na barabara kuu iendayo Dar es salaam.
Mgawanyo: Mji wa Serikali umegawanyika katika maeneo tofauti kama ifuatavyo:-
  • Wizara za Serikali, 
  • Ofisi za Mabalozi, 
  • Nyumba za Serikali, 
  • Huduma za Jamii, 
  • Maeneo ya biashara,
  • Bunge, 
  • Mahakama, 
  • Maegesho ya magari, 
  • Eneo la majitaka
Mifumo ya Maji: Mji wa Serikali utakuwa unatumia maji lita za ujazo 3,016.7 kwa siku. Mfumo wa majitaka utakuwa umeunganishwa na mtambo wa kisasa utakaofanya kazi ya kupokea majitaka na kuyachakata kuwa maji safi tena kwa ajili ya matumizi mengine.
Gharama: Gharama za Utekelezaji ujenzi wa Mji wa Serikali: Makadirio ya gharama za kukamilisha Mji wa Serikali ni Dola za Kimarekani 4,788,749,111 sawa na Shilingi za Kitanzania Trilioni 10,709,176,758,503. Gharama hizi zinategemewa kutoka katika vyanzo mbalimbali vifuatavyo:-
  • Fedha za Serikali, 
  • Wafadhiri, 
  • Mashirika ya Umma, 
  • Taasisi binafsi na za serikali, na 
  • Mashirika binafsi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages