Ligi ya soka ya wanawake nchini Ujerumani inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 29, lakini bila ya mashabiki. Shirikisho la soka la Ujerumani, DFB limetangaza hatua hiyo jana baada ya ligi hiyo kusimamishwa kwa takriban miezi mitatu kutokana na janga la virusi vya corona.
Ligi ya wanaume ilirejea wiki iliyopita, pia bila ya mashabiki uwanjani na chini ya vizuizi vikali vya kiafya vilivyotengenezwa kwa lengo la kupunguza kusambaa kwa maambukizi.
Rais wa DFB Fritz Keller ameeleza kufurahishwa na hatua hiyo na kusema huo ndio mshikamano unaohitajika hasa katika kipindi hiki cha mzozo.
Klabu 11 kati ya 12 zilipiga kura ya kuunga mkono kurejeshwa kwa ligi, lakini timu ya Cologne haikupiga kura.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇