Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un hatimaye amejitokeza hadharani katika uzinduzi wa kiwanda cha mbolea Ijumaa Mei 1 baada ya uvumi kuhusu afya yake, limesema shirika la habari la serikali la KCNA.
Shirika la habari la KCNA limesema wafanyakazi katika kiwanda cha mbolea walianza ," kushangiliia kwa nguvu" wakimshangilia Kim, ambao shirika hilo lilisema , analiongoza taifa hilo katika mapambano ya ujenzi wa uchumi wa kujitegemea kutokana na "upepo mkali unaokuja" kutoka kwa "nguvu hasimu.
Vyombo vya habari vya taifa viliripoti kwamba Kim anafanya shughuli za kawaida bila kutoka hadharani, kama kutuma salama kwa viongozi wa Syria, Cuba na Afrika Kusini na kuelezea shukurani zake kwa wafanyakazi wanaojenga maeneo ya kitalii katika mji wa pwani wa Wonsan, ambako baadhi ya watu walisema anaishi huko.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un hajahudhuria sherehe rasmi ya Aprili 15, sio kwa sababu ya hali yake ya kiafya, lakini kama hatua ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya janga la Covid-19, waziri mwenye dhamana ya muungano wa Korea Kusini alisema mapema wiki hii.
Kukosekana kwa kiongozi huyo wa Korea Kaskazini wakati wa sherehe hii ya kijadi ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa babu yake Kim Il-sung, mwanzilishi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, haijawahi kutokea na hajawahi kuonekana hadharani tangu wakati huo, hali ambayo ilichochea uvumi kuhusu hali yake ya afya. CHANZO: RFI
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇