LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 25, 2020

KIGOMA WAAHIDI KUMPA RAIS DK. MAGUFULI ASANTE YA KURA ZA KISHINDO 2020 KWA DHAMIRA YAKE YA KUFUFUA ZAO LA MICHIKICHI MKOANI HUMO

Na Hamis Shimye, Kigoma
UAMUZI wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli kudhamiria kufufua zao la mchikichiki ni hatua madhubuti inayokwenda kubadilisha hali na maisha ya mwananchi hasa wa Kigoma ambaye zao la mchikichi ni tegemeo la maisha yake.

Tumekuwa kwa zao hilo na hata wazazi wetu wamesoma shule kwa zao hilo ambalo kwa miaka ya nyuma ndio lilikuwa zao kubwa sana na ndio maana kwenye kila kaya ndani ya mkoa wa Kigoma huwezi ukakosa kukuta mashine ya kukamua mawese kwa njia ya kienyeji.

Unapozungumzia zao la mchikichi, unazungumzia maisha ya wanaKigoma kwa kuwa ndio mzizi wa watu wa huko, hivyo uamuzi wa Rais Dk. Magufuli kuamua kuinua zao hilo, umetukuna sana hasa watu wa Kigoma kwa kuwa unakwenda kuondoa na kukata kiu ya umaskini wetu, ambao sasa naweza kusadiki unaondoka.

Rais Dk. Magufuli umefanya kitu cha heshima leo, hasa kwa uamuzi wako wa kumtuma Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kugawa bure miche bora milioni 1.8 kwa wakulima wa Mkoa wa Kigoma.  Japokuwa naamini hili kuna baadhi ya wanasiasa ucharwa watasema lao!. Hawa ni wa kupuuzwa.

Serikali ya awamu ya tano imetuinua katika mambo mengi iliyoyafanya kwa mkoa mzima wa Kigoma, lakini hili la zao la mchikichi Kigoma ni hatua bora zaidi kwa kuwa linagusa maisha ya mtu mmoja mmoja kwenye kila kaya kwa kuwa toka tukiwa wadogo tunaona wazee wetu walivyokuwa wanatilia msukumo wa zao hilo.
Busara na hekima ya serikali ya awamu ya tano kwa uamuzi huu, nadhani huu ndio wakati wananchi wa Kigoma hasa wa Kigoma Kaskazini kuona fursa hii imekuja kwao katika kuwapambania na kuwakwamua kuondokana na umaskini na sasa ni wakati wa kukifanya kilimo bora cha zao la michikichiki kwa mkoa mzima wa Kigoma. 

Tanzania inatajwa kuwa miongoni mwa nchi duniani zenye mazingira mazuri ya uzalishaji wa michikichiki lakini inakadiriwa kuwa inaagiza tani zisizopungua 400,000 za mafuta ya mawese kila mwaka hasa kutoka Malaysia ili kufidia pengo la uhaba wa mafuta, licha ya uwezo wa uzalishaji wa mbegu zingine za mafuta. 

Kwa mujibu wa kitabu cha hali ya uchumi wa Taifa cha mwaka 2017, uzalishaji wa mazao ya mbegu za mafuta ya alizeti, karanga, ufuta, mawese na soya uliongezeka hadi tani 6.6 milioni kutoka tani 6.3 milioni mwaka 2016, sawa na ongezeko la asilimia 5.8. Sasa tunakwenda kuweka historia kwa kuwa na Kiongozi mtendaji. 

Zao la mchikichi limekuwa mkombozi kwa wakulima wengi wa Mkoa wa Kigoma kwani hutumika kwa chakula, biashara, mafuta ya mise hutumika katika mapishi ya vyakula mbalimbali pia husaidia mwili kupata nguvu na joto na hutumika katika utengenezaji wa sabuni na vipodozi mbalimbali. Na ndio maana nasadiki uamuzi huu unakwenda kututoa kwenye lindi la umaskini.

Chukulia kwa mfano nchi kama Indonesia na Malaysia ambazo zilitoa mbegu ya zao la mchickichi kutoka Mkoa wa Kigoma nchini Tanzania miaka ya 1960 kwa sasa zinaongoza kwa uzalishaji na usambazaji wa mafuta ya mawese na bidhaa zitokanazo na michikichi huku Tanzania ikiwa haina mafanikio yeyote hili haliwezekani.

Pia, Malaysia pekee huzalisha tani milioni 18.79 milion za mafuta ya mawese na kusambaza tani milion 18 za mazao yanayotokana na zao la michikichi duniani yakiwemo mafuta ya mawese ambayo Tanzania imekuwa ikiagiza takribani asilimia 65 ya mafuta ya mawese kutoka nchini ya Malaysia, zikifuatiwa na nchi nyingine ikiwemo Thailand.

Kwa ukanda wa Afrika nchi za Nigeria, Kenya, Ghana, Cameroon na Benin zinatajwa kuongoza katika uzalishaji wa zao la mchikichi ambapo nchi ya Nigeria huzalisha tani milioni 2.3 ya mafuta ya mawese kwa mwaka na kuifanya kuwa nchi ya tatu kwa uzalishaji kidunia na ukilinganisha fursa na upatikanaji wa zao hilo nchini.

Kutokuwepo kwenye rekodi ya uzalishaji wa zao hilo inauma hasa ikizingatia sababu kubwa zinazofanya zao hili kutojulikana na kutomnufaisha mkulima wa kawaida nchini Tanzania ni teknolojia duni ya kilimo cha zao hili na ukosefu wa miundombinu ya kuchakata mazao yatokanayo ya mchikichi hususan viwanda, ambapo naamini baada ya kugawa kwa miche hii sasa ni safari ya kuelekea kulipa thamani zao hilo.

Rais Dk. Magufuli umetupa heshima na kawaida ya sisi wanaKigoma ni waungwana na kwa hili tunakuambia tena AKHSANTE sana ni mjinga tu atakayekupinga 2020 na tunakuomba sana katika uchaguzi wako, utatukuta Mahembe uwanjani tukikusubiri kukupa kura za NDIYO maana umetupa ngazi ya kuondokana na umaskini wetu. 

Hamis Shimye
Mahembe, Kigoma Kaskazini

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages