Mbunge wa Kawe, Halima Mdee anayekabiliwa na kesi ya uchochezi wa kutoa maneno ya kuudhi dhidi ya Rais John Magufuli, amekutwa na kesi ya kujibu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hatua hiyo inatokana na uamuzi uliotolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Hakimu Simba amesema kuwa mahakama hiyo imemkuta Mdee na kesi ya kujibu na kwamba anatakiwa kuwasilisha utetezi wake mahakamani hapo.
Uamuzi huo umetokana na Upande wa Mashtaka kufunga ushahidi wake Februari 20, 2020 .
Mdee kupitia wakili wake Hekima Mwasipo amedai kuwa mteja wake atajitetea kwa kiapo na atakuwa na mashahidi watano.
Inadaiwa kuwa Julai 3, 2017, katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni, Mdee anadaiwa kutamka maneno dhidi ya Rais John Magufuli.
Mdee alifikishwa mahakamani hapo Julai 10, 2017, na kushtakiwa kwa mashtaka ya uchochezi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇