LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 16, 2020

DAWA YA CORONA KUMBE ALIKUWA NAYO RAIS MAGUFULI...AHSANTE KWA KUTUPONYA WATANZANIA


Na Said Mwishehe,Michuzi TV

RAIS Dk.John Magufuli naomba nianze kwa kukusalimia mzee wangu.Shikamoo,natumai unaendelea vema na jukumu la  kuwatumikia Watanzania na hasa ya kuleta maendeleo yao.

Baada ya salamu iliyoambatana na unyenyekevu mkubwa kwako naomba sasa nieleze jambo japo kidogo tu.Ndio kuna kitu nataka kueleza na linahusu janga la virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid- 19.

Kama mnavyofahamu ugonjwa huo bado umeendelea kuwa tishio duniani kote.Mataifa madogo na makubwa kiuchumi yanalia.Corona imeharibu kila kitu Duniani. Imeharibu maisha ya watu kwa kusababisha vifo.Imeharibu maisha ya watu kwa kuharibu shughuli za kiuchimi.

Corona imeharibu maisha ya watu kwa kusababisha maisha ambayo hayakuwa ya aina hiyo hapo awali kabla ya ugonjwa huo.Ndio Corona imevuruga kila kitu kwenye maisha yetu.Wenye ule utamaduni wa kusalimiana kwa kushikana mikono leo hawana hiyo nafasi.Tunaogopa.

Tumeambiwa tusishikane mikono kwani tunaweza ambukizana virusi. Rais Magufuli alikuwa wa kwanza kuonesha mfano.Unakumbuka Maalim Seif Sharif Hamad alipokwenda Ikulu kuonana na Rais walivyosalimiana.Hawakushikana mikono bali waligongesha miguu yao kama ishara ya kusalimiana

Wakati nikiendelea kutafakari ugonjwa huo naomba nikumbushe kidogo, Shirika la Afya Duniani( WHO)limetoa taarifa ya kwamba kuna uwezekano mkubwa Corona kuendelea kuwepo hapa duniani.Kwa lugha nyingine Corona haitamalizika siku za karibuni.Ipo na itaendelea kwa miezi kadhaa ijayo.Ndio walivyosema.

Swali la kujiuliza hivi kama kweli Corona bado tunayo kwa muda mrefu nchi ambazo zimefungia watu ndani na kusimamisha shughuli zote za kiuchumi watafanya hivyo hadi lini? Mataifa makubwa yakiwemo ya Marekani na Uingereza yanaumiza kichwa kutokana na uwepo wa Corona. Wameweka Lockdown kama hatua ya kukomesha kuenea kusambaa kwa Corona lakini hali imekuwa mbaya.

Kwangu mimi ukiniuliza kati ya Tanzaia na Marekani wapi wamefanikiwa kukabiliana vilivyo na Corona ,jibu langu litasimama kwa Tanzania.Ukweli Tanzania chini ya Rais Dk.Magufuli imefanikiwa kuidhibiti Corona.Mwanzoni Dunia ilikuwa haijamuelewa Rais Magufuli lakini leo hii wamekubali Rais Magufuli aliona mbali.

Rais Magufuli kitaaluma ni mwanasayansi aliyebobea zaidi kwenye mambo ya Kemia. Hivyo kwenye hili la Corona anachokieleza anakijua.Yeye kwenye hili la janga la Corona anaouwezo mkubwa wa kulizungumzia kuliko wengine.

Kuna Marais ambao sio wanasayansi,hivyo wanategemea maelekezo ya wanasayansi waseme na kisha wao ndio waseme.Kwa Dk.Magufuli ni tofauti yeye na wanasayansi wenzake kwenye kukabiliana na Corona wanakaa meza moja kutafuta ufumbuzi.

Ndio maana kwa Tanzania chini ya maelekezo yake kwa kushirikiana na watalaam wake, tumefanikiwa kukabiliana na Corona.Tunafahamu Corona bado ipo na itaendelea kuwepo.

Wakati WHO wanatueleza leo kuwa Corona itaendelea kuwepo, Rais Magufuli alishaliona hilo muda mrefu na alishwaambia Watanzania kuhusu kuendelea kuwepo kwa ugonjwa huo kwa muda mrefu.Rais Magufuli aliiambia Dunia kuhusu changamoto za vipimo vya Corona katika kutoa majibu.

Leo Marekani nao wanapita mule mule ambao Rais Magufuli alisema.Katika janga la Corona Tanzania ni mahali salama pa kuishi kukiko Marekani.Unashangaa nini? Angalia takwimu za idadi ya waliokufa Marekani na kisha rejea Tanzania.

Hebu tuachane na hayo.Najua wapo wanaokereka kwa kueleza ukweli.Niwaambie kwenye hili mtakereka sana.Kwangu sioni kama Marekani ni sehemu salama.Sio pakukimbilia katika kipindi hiki cha Corona. Nchi salama kwa sasa ni Tanzania.Hata ukinuna haisaidii na huo ndio ukweli.

Tanzania ni nchi pekee iliyoamua kufuata mfumo wake kukabiliana na Corona. Wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila siku.Corona inapita kushoto na sisi tunapita kulia.Siku zinakwenda bila tatizo.Hakika Mungu anao mpango mzuri na Tanzania.Ahsante Mungu kwa kuweka mkono kwenye Corona.Wakati wengine wanajifungia ndani ,Tanzania watu wanaendelea kuchapa kazi.Ni mwendo wa Hapa Kazi Tu.

Sasa naomba nikwambie kitu,huenda tangu mwanzo nilichoeleza hujaniliewa.Kwangu hilo sio tatizo, najua tunatofautiana kwenye kuelewa.Tufanye hivi elewa kuanzia hapa.Juu achana nako kama nimekuchosha.

Iko hivi mataifa mbalimbali  Duniani yanahaha kutafuta dawa ya Corona bila mafanikio. Kwa nchi ya Madagasca angalau wamepata mwanga.Wanayo dawa yao ya kutibu Corona.WHO wameipinga lakini wenyewe Madagasca hawana nongwa wanaendelea nayo.Inawasaidia.

Tanzania chini ya Rais Magufuli waliamua kuifuata dawa hiyo.Kwa sasa inafanyiwa utafiti,ikithibitika kufaa hata mimi nitakunywa.Ndio!Mbona unakodoa macho.Wewe subiri itakayothibishwa na WHO.Hata hivyo tayari NIMR nao wanayo dawa yao, itatufaa kwa kipindi hiki.

Wakati Dunia ikiendelea kutafuta dawa ya Corona, Tanzania  imepata bahati kubwa sana kwani angalau kupitia Rais Magufuli amesaidia kututibu kwa dawa yake.Unaweza kuuliza ni dawa ya aina gani? Jibu ni kwamba hotuba yake aliyoitoa hivi karibuni akiwa Chato imewatibu Watanzania wengi waliokuwa wakisumbuliwa na Corona.

Kwangu naweza kuitofautisha Corona kwa namna mbili. Aina ya kwanza ni wale wanaogua Corona kwa kuwa na virusi.Kundi hilo watu wake wanahesabika kwani takwimu zipo.Wakati kundi la pili wanaougua Corona ni wale ambao hawana virusi vya ugonjwa huo lakini walitawaliwa na hofu.

Waliokuwa wanaugua Corona kwa maana ya hofu walikuwa wengi  kuliko wenye virusi vya Corona.Rais Magufuli alitambua ukubwa wa hofu kwa watu wake.Hivyo akaamua kutoa hutuba mujarabu ambayo imetosha kuwa dawa kwa Watanzania. Ukweli kabla ya hotuba ya Rais hofu kuhusi ugonjwa huo ilikuwa kubwa.Binafsi hata mimi nilikuwa nimejawa hofu.

Katika mitandao ya kijamii nako uzushi ulikuwa mkubwa sana.Wazushi wakasababisha hofu.Kila mahali ikawa hofu.Hofu hiyo iliyondoka tu baada ya  hotuba ya  Rais Magufuli.Hakika hotuba ya Rais wetu Dk.Magufuli imetibu wengi .Imetibu kila mtu aliyekuwa na hofu ya ugonjwa huo.

Wakati baadhi ya viongozi wa nchi nyingine wakiendelea kuwajengea hofu wananchi wao kwa kuendelea na Lockdown kwa Tanzania Rais kipenzi cha watu anatumia nafasi yake kutoondolea hofu.Wakati wa hotuba yake Rais Magufuli alizungumza kwa kina madhara yatokanayo na hofu.Aksema hofu inaua kuliko ugonjwa wenyewe. Ametuondoa hufu na hakika ndio dawa pekee iliyokuwa inahitajika kwa sasa wakati watalaamu wakiendelea kutafuta dawa sahihi.

Rais Magufuli katika hotuba yake amewakumbusha Watanzania kuendelea kufuata maelekezo yanayotolewa kuhusu kukabiliana na Corona.Ameendelea kusisitiza ugonjwa upo , hivyo kuchukua hatua za kukabiliana na Corona.Akaweka msisitizo hakuna sababu ya kutishana bali kila mmoja wetu kuchukua tahadhari ya kujikinga.Akasema ugonjwa huo na hauna tofauti na magonjwa mengine ambayo wakatii yanaingia watu walikuwa na hofu na sasa yamekuwa magonjwa ya kawaida na tunaishi nayo.

Hotuba ya Rais hakika imekuwa tiba tosha kwa Watanzania walio wengi.Tangu atoe hotuba yake Watanzania wamekuwa na amani ya moyo.Hawana hofu. Corona pamoja na kuwa ugonjwa unoogopewa kwa walio wengi baada ya hotuba ya Rais  hakuna anayeogopa tena.Ukifuatilia huko mtaani hata vibarakoa vinavaliwa chini ya pua.Watu hawana hofu tena.Hata hivyo jambo nzuri ni kuona namna ambavyo Watanzania wameendelea kuchukua tahadhari kama Rais alivyosisitiza katika hotuba yake.

Kwa mtazamo wangu hotuba ya Rais Magufuli imekuwa tiba tosha kwetu.Kuna wakati nawaza dawa ya Corona kumbe alikuwa nayo Rais Magufuli, ahsante kwa kutoponya.Kubwa kuliko yote mataifa mengi yanapaswa kujifunza kutoka kwa Rais Magufuli kuhusu namna ya mbinu bora na sahihi kukabiliana na Corona.Tuendelee kuchukua tahadhari ,jikingine,wakinge na wengine.

Kwa mawasiliano 0713833822

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages