Na Shukrani Kawogo, Njombe
Imeelezwa kuwa kutokana na wanafunzi kuwepo katika kipindi hiki cha likizo kutokana na ugonjwa wa Corona imepelekea wanafunzi hao kuzagaa vichakani na kujihusisha na masuala ya kimapenzi kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya wanafunzi hao.
Hayo yameelezwa na wananchi wa Kata ya Ibumi wilayani Ludewa Mkoani Njombe katika mkutano wa kujadili maenendeleo ya kata hiyo ulioongozwa na diwani wao Edward Haule ambaye pia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Aidha diwani huyo amesema kuwa wanafunzi watakaokamatwa katika vichaka hivyo wote kwa pamoja wakiume na wakike watafikishwa kituo cha polisi na ikiwezekana wachapwe viboko ili iwe fundisho na kwa wengine,
“Nilazima itolewe adhabu kwa wote waliokamatwa na si kuwakamata watoto wa kiume tu halafu wakike waachwe hapo tutakuwa hatujatatua tatizo kwani huyu wakike ambaye haadhibiwi atamfariji mwenzie baada ya adhabu kisha mambo yakaendelea, hivyo wote wakiadhibiwa hakutakuwa na wakumfariji mwenzie”, Alisema Diwani Haule.
Aliongeza kwa kuwataka wazazi na walezi kutoa ushirikiano wa kutosha pindi yanapotokea masuala kama haya ili kunusuru mimba za utotoni pamoja na matokeo mabaya katika mitihani yao.
Hata hivyo kwa upande wa mmoja wa wananchi hao aliyefahamika kwa jina la Mussa mkatakulima ameuomba uongozi suala hilo lichukuliwe kwa uzito wake na kwa yeyote atakayebainika sheria ichukue mkondo wake.
“ Kumekuwa na mahusiano ya wanafunzi kwa wanafunzi wengine ni watu wazima wanajihusisha kimapenzi na wanafunzi na wanapobainika wanayamaliza kwa kuzungumza kawaida tu! Mimi naomba sheria ichukue mkondo wake maana tukileana sana tunapeana kilema”, Alisema Mkatakulima.
Diwani wa kata ya Ibumi iliyopo wilayani Ludewa Mkoani Njombe, ambaye pia ni mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Edward Haule akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na wananchi
Baadhi ya wananchi wa kata ya Ibumi wakimsikiliza Diwani wao Edward Haule
Diwani wa kata ya Ibumi iliyopo wilayani Ludewa Mkoani Njombe ambae pia ni mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Edward Haule(aliyesimama) akizungumza na wananchi wa kata yake.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇