Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli rasmi ameruhusu kufunguliwa kwa Vyuo vyote June 1, 2020 pamoja na Michezo ikiwemo Ligi Kuu mbalimbali kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa Maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID-19).
Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo Ikulu - Chamwino jijini Dodoma alipokuwa anawaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni, Rais Magufuli ameagiza Wizara ya Elimu na Fedha kuhakikisha Wanafunzi hao wa Vyuo wanaorejea Vyuoni humo wanapatiwa Mikopo yao kwa muda mchache uliobaki.
Pia Rais Magufuli ameagiza Wizara ya Afya kuratibu utaratibu maalum kwa Wanamichezo inaporejea June 1 ili kuhakikisha tahadhari inaendelea kuchukuliwa dhidi ya Maambuzi ya Virusi vya Corona ambavyo vimepungua kwa kiasi kikubwa hapa nchini.
Kuhusu Shule za Msingi na Sekondari, Dkt. Magufulia ameagiza Shule hizo kujipa muda kidogo kuangalia hali ya Maambukizi ikoje katika kipindi hiki maambukizi hayo yanaendelea kupungua zaidi.
"Wanafunzi Shule za Sekondari na Msingi tuzipe muda kidogo, hawa Wakubwa wanaelewa ziadi kuhusu masuala ya Maambukizi, sisi wa huku tujipe muda kidogo", amesema Rais Magufuli.
Aidha, Dkt. Magufuli ameagiza Mamlaka zinazohusika na masuala ya Utalii kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ujio wa Watalii hapa nchini ifikapo May 27-28, 2020 sambamba na kuruhusu Ndege za Watalii hao kutua nchini. "Wakitaka kuja kujifukiza na Nyungu waje tu", ameeleza Dkt. Magufuli.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇