LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 7, 2020

WAZIRI MKUU BORIS JOHNSON APELEKWA ICU

  Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amepelekwa katika chumba cha kuhudumia wagonjwa mahututi ICU baada ya hali yake kiafya kuwa mbaya kwa siku kumi zaidi kwasababu ya ugonjwa wa virusi vya Corona, kwa mujibu wa msemaji katika makazi ya Waziri Mkuu.

Johnson amemuambia Waziri wa mambo ya nje Dominic Raab kuchukua usukani pale ambapo kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo.

Waziri Boris ,mwenye umri wa miaka 55, alilazwa katika hospitali ya St Thomas mjini London wakati hali yake ya kiafya ilipokuwa haina ahueni huku homa na kukohoa kukiongezeka zaidi siku ya Jumapili. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya ushauri kutoka kwa timu yake ya matibabu na anaendelea kupata huduma stahiki.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages