Serikali kwa kushirikiana na wadau imeandaa na kuanza kutekeleza Mpango-Kazi wa Kitaifa wa Kupunguza Matumizi ya Zebaki kwa Wachimbaji Wadogo wa Dhahabu (2020 – 2025).
Hayo yamesemwa jana April 16 Bungeni jijini Dodoma na Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Makamu Wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu wakati akiwasilisha hotuba Kuhusu Makadirio Ya Mapato Na Matumizi Kwa Mwaka 2020/21 .
Waziri Zungu amebainisha kuwa Mpango-Kazi huo unalenga kupunguza matumizi ya Zebaki kwa asilimia 30 ifikapo 2025.
Waziri Zungu amesema Wizara yake ilitoa elimu kwa umma kuhusu madhara yatokanayo na Zebaki kwa afya ya binadamu na mazingira hususan katika maeneo ya wachimbaji wadogo wa dhahabu ikiwemo mikoa ya Mara, Geita, Shinyanga na Singida .
Aidha Waziri Zungu amefafanua kuwa Wizara yake itaendelea kuratibu utekelezaji wa Mkataba wa Kupambana na Kuenea kwa Hali ya Jangwa na Ukame ikiwa ni pamoja na kukamilisha maandiko mawili (2) ya miradi na kuwasilisha kwenye Sekretarieti ya Mkataba.
Katika ufuatiliaji wa Katazo la utumiaji wa Mifuko ya plastiki ,
Mhe.Zungu amesma jumla ya tani 259.2 za mifuko ya plastiki
zilikusanywa, kati ya hizo tani 86.7 zilirejelezwa kwenye viwanda mbalimbali, na tani 172.5 ziliteketezwa.
Kuhusu utekelezaji wa majukumu yake Waziri Zungu amesema Ofisi yake ilikumbana na changamoto kadhaa zikiwemo Upungufu wa idadi inayostahili ya watumishi katika kusimamia shughuli za Muungano na Mazingira; Kukosekana kwa Mfumo Thabiti wa Mashirikiano baina ya Taasisi za Serikali kuhusu Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira pamoja
na Uelewa Mdogo wa Jamii kuhusu Uhifadhi na Usimamizi wa Masuala ya mazingira.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda ,Biashara na Mazingira Suleiman Ahmed Saddiq ameishauri Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira kuongeza juhudi katika Kukamilisha mchakato wa mapitio ya Sera ya Taifa ya Mazingira 1997 na mkakati wa utekelezaji wake kwa lengo la
kuihuisha iendane na mazingira halisi ya sasa na iweze kuboresha usimamizi wa shughuli za mazingira.
Wizara ya Nchi Ofisi Ya Makamu Wa Rais Muungano na Mazingira imeomba kuinidhishiwa Jumla ya Shilingi bilioni ishirini na saba , milioni mia tisa tisini , laki moja na hamsini na tano elfu [[Tsh.27,990,155,000] kwa ajili ya utekelezaji wa Majukumu mbalimbali ya Wizara.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇