LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 1, 2020

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKETE AGUSWA NA KIFO CHA KATIBU MKUU CUF


Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, ameonesha kuguswa na msiba wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Khalifa Suleiman, aliyefariki Dunia usiku wa kuamkia leo na kusema kuwa amepoteza rafiki yake wa muda mrefu.

Dkt Kikwete ameyabainisha hayo leo Machi 31, 2020, kupitia ukurasa wake wa Twitter, na kutoa pole kwa Mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na wanachama wote na kwamba wamepoteza kada wa kuaminiwa na kutumainiwa.

"Ni kweli tulikuwa pande mbili tofauti, lakini kama wanadamu tulikuwa marafiki tangu wakati tukiwa wote bungeni na hata baada ya mimi kuacha Ubunge, daima nitamkumbuka kwa moyo wake wa upendo, ukarimu, ucheshi na huruma, tuko pamoja katika majonzi na kuomboleza, tunakuombea wewe binafsi, wanachama wote wa CUF na familia ya marehemu moyo wa subira na ustahamilivu. Innalilahi Wainna Ilaihi Rajiun" ameandika Dkt Kikwete.





Poleni sana Mwenyekiti Ibrahim Lipumba na wanachama wa CUF kwa msiba mkubwa wa Mheshimiwa Khalifa Khalifa uliowakuta. Ni msiba wetu sote. Mmepoteza kiongozi na Kada wa CUF wa kuaminiwa na kutumainiwa. Mimi nimepoteza rafiki wa muda mrefu.


View image on Twitter
Ni kweli tulikuwa pande mbili tofauti lakini kama wanadamu tulikuwa marafiki tangu wakati tukiwa wote Bungeni na hata baada ya Mimi kuacha Ubunge.

Daima nitamkumbuka kwa moyo wake wa upendo, ukarimu, ucheshi na huruma. Tuko pamoja katika majonzi na kuomboleza.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages