Mbunge wa Jimbo la Rombo, Joseph Selasini, leo Aprili 28, 2020 ametangaza rasmi kukihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kujiunga na chama cha NCCR-Mageuzi baada ya kumalizika kwa vikao vya Bunge.
Jana, Selasini alidai kutengwa na wabunge wenzake wa chama chake cha CHADEMA ikiwemo kuondolewa bila kupewa taarifa kwenye 'Group la WhatsApp' la Wabunge wa chama hicho ambalo pia yumo Mwenyekiti wa chama Freeman Mbowe
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇