BUSEGA, Simiyu
MKUU wa Wilaya ya Busega iliyopo Mkoani Simiyu ametoa ujumbe wa Pasaka kwa Wananchi wote na kuhimiza wananchi kuzingatia tahadhari zinazotolewa na Wataalamu wa Afya.
"Nachukua nafasi hii kuwatakia Kheri ya Pasaka wana Busega na Watanzania wote kwa ujumla.
Tusherehekee sikukuu zetu kwa uangalifu mkubwa huku tukifata maelekezo ya Wataalam wetu wa Afya, epuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima, tuzingatie kunawa mikono kila wakati, au kutumia vitakasa mikono ( sanitizer).
"Kaa nyumbani kama huna safari ya lazima, Nenda katika ibada na haraka sana rudi Nyumbani huu sio muda wa kupiga stoi na marafiki, na wala sio muda wa kukaribisha wageni nyumbani kwako. Kila mtu akae kwake, watu zaidi ya watatu tayari ni mkusanyiko.
DC Tano Mwera amewahimiza Wananchi wa Busega kuongeza umakini na hata kuvaa barakoa (Mask) ikibidi kwani virusi hivyo pia usambaa kwa njia ya hewa.
"Taarifa mpya zinasema ugonjwa huu wa Corona (COVID 19) unaambukizwa pia kwa njia ya hewa hivyo umakini zaidi unahitajika, ikiwezekana vaa Barakoa.
"Kila mmoja kwa Dini yake tuendelee kumuomba Mungu atuepushie janga hili linalosababishwa na virusi vya Corona.
Pasaka Njema wote na Mungu awalinde. #Stayhome #HappyEaster " alimalizia DC Tano Mwera.
Your Ad Spot
Apr 12, 2020
DC TANO MWERA ATUMA UJUMBE WA PASAKA, ATOA TAHADHARI DHIDI YA CORONA BUSEGA
Tags
Corona#
featured#
Share This
About Bashir Nkoromo
featured
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇