Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiishukuru Kampuni ya Barrick kwa kuiunga mkono serikali katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George.
(PICHA NA MALUNDE-MALUNDE 1 BLOG)
Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu ya Barrick kupitia Mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama imetoa msaada vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 48 kwa ajili ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona ‘Covid 19’ katika mkoa wa Shinyanga.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa leo Ijumaa Aprili 17,2020 na Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack.
Dkt. Antoinette amevitaja vifaa walivyotoa kuwa ni pamoja na Matanki ya kuoshea mikono ‘washing container set’ 88,goggles 40,Impermiable suits 40,Barakoa (face masks) 400, Vipimia joto (contact less thermometer) 6, Hand wash unit,Chlorine powder na chemical gloves jozi 50.
Dkt. Antoinette amesema Kampuni ya Barrick iko bega kwa bega na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona ndiyo maana imechangia vifaa hivyo ili kuwakinga wananchi dhidi ya Corona.
“Kinga ni bora kuliko tiba .Tumekabidhi vifaa vya kujikinga na Corona kwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ili vikatumike kukabiliana na Corona katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu ikiwemo masoko,vituo vya mabasi,minada,vituo vya afya na tutaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Corona”,amesema Dkt. Antoinette.
“Leo tumekabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 48 lakini Kampuni ya Barrick imetoa jumla ya shilingi Bilioni 4 zingine kukabiliana na Corona nchini Tanzania ambapo mkoa wa Shinyanga umetengewa shilingi milioni 600”,ameongeza Dkt. Antoinette.
Akipokea vifaa hivyo,Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ameishukuru Kampuni ya Barrick kwa kuiunga mkono serikali katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona huku akibainisha kuwa ni jukumu la kila mwananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.
“Tunawashukuru sana Barrick Buzwagi kwa mchango wenu,tutavigawa vifaa hivi katika maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga ili kama atapatikana mgonjwa basi tuweze kuokoa maisha ya mgonjwa.Maandalizi haya tunayafanya kama binadamu lakini tuendelee kumuomba Mungu atuepushie ugonjwa huu na tuwaombee waliopata maambukizi wapone ili maambukizi yasiwepo”,amesema Telack.
“Kila mtu achukue tahadhari,kunawa mikono maji safi yanayotiririka na sabuni ndiyo silaha yetu kubwa, ambayo tunajivunia, nawa ukiwa nyumbani, nawa ukiwa katika biashara zako,nawa ukiwa kazini,nawa kila wakati” ,amesema
Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa amewataka wananchi kuendelea kutoa taarifa za wageni wanaofika katika maeneo yao huku akisisitiza kuwa serikali itaendelea kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaoleta mzaha kuhusu ugonjwa wa Corona.
Naye Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha amesema sasa wananchi wengi wana muamko wa kutosha kuhusu ugonjwa wa Corona na kwamba changamoto bado ipo kwenye maeneo ya Baa na Klabu ambazo zinaendelea kukusanya watu pamoja na waendesha bodaboda wanaopakiza watu zaidi ya mmoja ‘mishikaki’.
Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kushoto) msaada vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 48 kwa ajili ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona ‘Covid 19’ katika mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Aprili 17,2020.
Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kushoto) msaada vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 48 kwa ajili ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona ‘Covid 19’ katika mkoa wa Shinyanga.
Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George akivitaja vifaa vilivyotolewa na Barrick Buzwagi kukabiliana na Ugonjwa Corona mkoani Shinyanga kuwa ni Matanki ya kuoshea mikono ‘washing container set’ 88,goggles 40,Impermiable suits 40,Barakoa (face masks) 400, Vipimia joto (contact less thermometer) 6, Hand wash unit,Chlorine powder na chemical gloves jozi 50. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akinawa mikono katika moja ya Matanki 88 yaliyotolewa na Mgodi wa Barrick Buzwagi yatakayowekwa katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi ikiwemo Vituo vya mabasi,minada,sokoni na vituo vya afya. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George.
Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George akinawa mikono katika moja ya Matanki 88 yaliyotolewa na Mgodi wa Barrick Buzwagi yatakayowekwa katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi ikiwemo Vituo vya mabasi,minada,sokoni na vituo vya afya.
Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kushoto) vifaa kwa ajili ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona ‘Covid 19’ katika mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kushoto) vifaa kwa ajili ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona ‘Covid 19’ katika mkoa wa Shinyanga. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha.
Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kushoto) vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 48 kwa ajili ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona ‘Covid 19’ katika mkoa wa Shinyanga. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiishukuru Kampuni ya Barrick kwa kuiunga mkono serikali katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama mgodi wa Barrick Buzwagi, Dkt. Antoinette George.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akionya kuhusu watu wanaoleta mzaha kuhusu Ugonjwa wa Corona na kubainisha kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akisisitiza umuhimu wa kila mwananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akielezea hatua zinazoendelea kuchukuliwa na serikali wilayani Kahama katika kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona ikiwa ni pamoja na kusititiza wananchi kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni lakini pia kuepuka mikusanyiko ya watu.
Meneja wa Mahusiano na Maendeleo ya Jamii mgodi wa Barrick Buzwagi, Siama Paul akielezea namna mgodi huo unavyoshiriki katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo amesema wamekuwa wakisambaza vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Corona,kutoa elimu kwa jamii kwa njia ya matangazo ya gari (Public Advertisement PA) na kutoa semina kwa watoa huduma za afya.
Meneja wa Mahusiano na Maendeleo ya Jamii mgodi wa Barrick Buzwagi, Siama Paul akielezea Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack namna mgodi wa Buzwagi unavyoshiriki katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo amesema wamekuwa wakisambaza vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Corona,kutoa elimu kwa jamii kwa njia ya matangazo ya gari (Public Advertisement PA) na kutoa semina kwa watoa huduma za afya. Wa pili kushoto ni Afisa Mahusiano mgodi wa Barrick Buzwagi Blandina Munghezi.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akimpima kiwango cha joto la mwili Mhe. Anamringi Macha (kulia).
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akimpima kiwango cha joto la mwili Meneja wa Mahusiano na Maendeleo ya Jamii mgodi wa Barrick Buzwagi, Siama Paul (kushoto).
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇