LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 31, 2020

“WELEDI NA KUJITUMA NDIO NGUZO YA MAFANIKIO”-DKT MWAKYEMBE


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayoub Rioba akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo la televisheni kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya utangazaji mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe lililotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Korea ambapo amesema kwa sasa jengo hilo ujenzi wake umefikia 20%. 

Waziri wa Habari Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa studio ya televisheni ya Taifa (TBC) kwa ajili ya uboreshaji wa mundombinu ya utangazaji. Kushoto ni Katibu Mkuu Habari, Dkt. Hassan Abbasi na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba. 
Waziri wa Habari, Dkt.Mwakyembe akiweka tofali kama ishara ya kuanza ujenzi wa studio za televisheni kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya utangazaji ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Jengo hilo linajengwa kwenye ofisi za TBC zilizopo Mikocheni Dar es salaam. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrrison Mwakyembe, Katibu Mkuu Habari Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba wakiwa kwenye picha ya pamoja na wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa jengo la televisheni ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) baada ya kuweka jiwe la msingi la kuanza rasmi ujenzi wa jingo hilo. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrrison Mwakyembe, Katibu Mkuu Habari Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba wakiwa kwenye picha ya pamoja na meneja pamoja na wakurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), baada ya kuweka jiwe la msingi la kuanza rasmi ujenzi wa jengo la studio la Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). 
Katibu Mkuu Habari, Dkt. Hassan Abbasi akiongea wakati wa hafla hiyo ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa studio mpya ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) inayojengwa katika eneo la ofisi hizo zilizopo Mikocheni. Programu Tumizi (App) ya Safari Channel, pamoja na mfumo mpya wa upashanaji habari unaofahamika kama TBC Aridhio. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 30 Machi,2020. 
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa studio mpya ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) inayojengwa katika eneo la ofisi hizo zilizopo Mikocheni. Programu Tumizi (App) ya Safari Channel, pamoja na mfumo mpya wa upashanaji habari unaofahamika kama TBC Aridhio. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 30 Machi,2020. 
Mwalimu wa Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Elizabeth Mahenge akizungumza wakati wa uzinduzi huo. Elizabeth Mahenge ndiye aliyekuja na neno ARIDHIO ambapo amesema neno ARIDHIO ni kisawe cha neno taarifa na pia ni kisawe cha neno Habari. 
Msanii Mrisho Mpoti akitoa burudani wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kwenye makao makuu ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizoko Mikocheni jijini Dar es salaam 
Waziri wa Habari, Dkt. Harrison Mwakyembe akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa Programu Tumizi (app) maalumu ya Chaneli ya Safari itakayokuwa ikipatikana kupitia playstore na IOS. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe,akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa studio mpya ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) inayojengwa katika eneo la ofisi hizo zilizopo Mikocheni. Programu Tumizi (App) ya Safari Channel, pamoja na mfumo mpya wa upashanaji habari unaofahamika kama TBC Aridhio. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 30 Machi,2020.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka watangazaji na watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kudumisha weledi na kujituma ili wengine wapate kuiga mambo mazuri kutoka kwao.

Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa studio mpya ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) inayojengwa katika eneo la ofisi hizo zilizopo Mikocheni. Aidha Dkt. Mwakyembe alizindua Programu Tumizi (App) ya Safari Channel, pamoja na mfumo mpya wa upashanaji habari unaofahamika kama TBC Aridhio ambapo neno Aridhio linamaanisha taarifa au habari.

“Tuna deni kubwa la kuhakikisha tunadumisha weledi na kujituma hivyo kuendelea kuwa kiongozi wa habari hapa nchini, lazima TBC kiwe ni chombo cha rejea,wakitangaza wengine mtu awe na shauku ya kujua TBC imesema nini kwanza”,amesema Dkt.Mwakyembe.

Kwa upande wake, katibu Mkuu wa Wizara ya habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amewapongeza wafanyakazi wa shirika hilo kwa hatua hiyo kubwa ya kuleta mapinduzi na ubunifu katika tasnia ya habari katika chaneli hiyo ya ya Tanzania inayotegemewa na taifa.

Mabadiliko haya makubwa ya upashanaji habari ndani ya TBC yanakuja baada ya miaka 13, ambapo safari hii ilianza mwaka 2007. Ujenzi wa jengo hilo la kisasa umeanza Februari, 2020 na utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.38/- na unatarajiwa kukamilika Agosti 2020, ambapo hadi sasa ujenzi huo umefikia asilimia 20.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo mpya wa upashanaji habari Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayoub Rioba amesema kuwa kutokana na mahitaji ya sasa ya dunia ya sayansi na teknolojia imelazimika mifumo ya zamani ya upashanaji habari kupinduliwa na kuja na namna mpya za upashanaji habari. Aidha Dkt. Ayoub Rioba ameishukuru Wizara kwa namna ambavyo imekuwa bega kwa bega katika kuunga mkono mafanikio ya Shirika hilo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages