Wizara ya Afya imetangaza kuwa, hadi sasa watu 11,679 waliokuwa wameabukizwa virusi vya ugonjwa wa COVID-19 au corona nchini Iran wamepata nafuu na kuruhusiwa kuondoka hospitalini.
Kianoush Jahanpour, Msemaji wa Wizara ya Afya ya Iran akizungumza Jumamosi na waandishi habari alisema: "Hadi sasa watu 35,408 nchini Iran wameambukizwa corona. Aidha ameongeza kuwa, hadi sasa idadi ya waliofariki kutokana na virusi hivyo kufikia adhuhuri ya Jumatano ilikuwa watu 2,517.
Ugonjwa wa COVID-19 uliibukia nchini China katika mji wa Wuhan mnamo Disemba 2019. Hivi sasa ugonjwa huo umeenea katika karibu nchi zote duniani.
Hadi kufikia sasa watu zaidi ya 606,000 wameambukizwa virusi vya COVID-19 duniani, wengi wao wakiwa nchini Marekani na walioaga dunia ni 30,880 wengi wao wakiwa nchini Italia.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇