LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 1, 2020

WAANDISHI WACHEZEA KICHAPO

Waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro akiwamo wa gazeti la Mwananchi, Janeth Joseph walijikuta katika wakati mgumu katika mkutano wa Mbunge wa Hai (Chadema), Freeman Mbowe baada ya askari polisi waliovaa sare na wengine kiraia kuwapiga kwa vitako vya bunduki walizokuwa wamebeba.

Kabla ya kutokea vurugu hizo, juzi katika mkutano wa Mbowe uliokuwa ukifanyika katika viwanja vya Nkoromu katika Kata ya Masama kati wilayani Hai, polisi walivamia gari la mbunge huyo wakitaka kuingia ndani kwa nguvu, ndipo mwandishi huyo aliyekuwa katika majukumu yake ya kazi akipiga picha alinyang’anywa simu na kisha wakaanza kumpiga.

Mwandishi mwingine aliyeshambuliwa na askari hao ni wa Global TV, Elia Peter.

Akizungumzia tukio hilo jana, Janeth alisema kabla ya kuanza kuchukua matukio katika mkutano huo alijitambusha kwa askari hao kuwa yeye ni mwandishi, hivyo akataka ushirikiano na askari hao.

‘’Tulipofika eneo la mkutano tulijitambulisha kwa askari waliokuwa eneo la viwanja vya Nkoromu kwamba sisi ni waandishi wa habari, nashaanga nikiwa nachukua matukio wakati Mbowe anazingirwa na askari hao, mmoja wao ambaye nimemtambua sura alinifuata akaninyanganya simu yangu’’

“Nilipomuuliza ni kwanini amechukua simu yangu wakati nilijitambulisha kwao kuwa mimi ni mwandishi wa habari, alivua silaha yake aliyokuwa amebeba na kuanza kunishambulia sehemu za kifuani.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages