LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 30, 2020

VISA VINNE VIPYA VYA CORONA VYATHIBITISHWA KENYA


Kulingana na waziri Kagwe visa vinne vilivyoongezeka vya COVID-19 vinalifanya taifa hilo kuwa na jumla ya visa 42, tangu kisa cha kwanza kiliporipotiwa tarehe 13 Machi.

Visa hivyo ni pamoja na Mkenya mmoja, raia mmoja wa Cameroon, Mmarekani mmoja na raia mmoja wa Burkina Faso . Akitoa taarifa kuhusu janga la coronavirus

Bwana Kagwe amewashauri Wakenya wote kushirikiana kuzuwia maambukizi ya corona badala ya kuuachia mzigo huo serikali pekee:'' Tunahitaji kufikiria jinsi ya kushughulikia tatizo hili kama serikali, jamii na kila mkenya'', amesisitiza Bwana Kagwe.

Amewaomba Wakenya kuwa tayari kwa hali yoyote inayoweza kujitokeza kutokana na virusi hivi na akasisitizia umuhimu wa waajiri kuwaruhusu wafanyakazi wao kuondoka kazini mapema kabla muda wa maruku ya kutotoka nje inayoanza saa moja jioni haijaanza kutekelezwa.

'Si haki kuwaachilia wafanyanyakazi muda wa kutotoka nje unakaribia, kama haitawezekana basi waajiri wawapatie malazi wafanyakazi wao'' amesema waziri Kagwe.

Aidha amehimiza kila Mkenya kusingatia usafi ili kuepuka maaambukizi ya coronavirus.

Waziri huyo amesema kuwa licha ya juhudi zinazofanywa na serikali kuimarisha miundombinu yake ili kuweza kukabiliana na maambukizi, Benki ya dunia imetoa pia msaada wa vfaa vya kusaidia wagonjwa kupumua(Ventilators) 250 na akasemajuhudi zinafanyika kupata vifaa zaidi vya matibabu.

''Kuanzia wiki ijayo tutaanza kutengeneza zana za watu kijilinda binafsi , Vitanda vya wagonjwa mahututi 1000 vitaongezwa kwenye hospitali zetu ICU birds-1000 beds zaidi. Tutaanza kutengeneza barakoa hivi karibuni.Kila siku tunaendelea kujenga uwezo wa vifaa vya kimatibabu'' amesema waziri Kagwe

Wakati huo wahudumu wa afya wanatazamiwa kuajiriwa katika kila hospitali kadr watakapohitajika ambapo Bwana Kagwe amesema serikali inataka kuwaajiri maafisa wa afya walau 1000 hivi karibuni. 
 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages