Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dkt. Respicious Boniface akizungumza jambo katika hafla fupi kabla yakupokea Misaada kutoka kwa Wanawake TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam leo Machi 6, 2020 kupitia viongozi wa matwi Kamati za Wanawake kutoka katika Hospitali husika kueleke Siku ya Wanawake Duniani itakayo fanyika Kitaifa Machi 8, 2020 Mkoani Simiyu,
Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kutujalia Afya njema kufikia siku ya leo tukiwa na afya njema na pia nami nimependeza kwa kuwezeshwa nanyi hakika Mungu awabariki sana sana tena sana muendelee kuwa na moyo wa huruma
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dkt. Respicious Boniface wakati akipokea misaada na alianza kwa kuishukuru Kamati ya Maandalizi wakiongozwa na Katibu TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Tabu Mambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake TUGHE kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) Rosemary Aaron
Nawapongeza kamati yote kwa kazi nzuri mnayoifanya na kwa MOI chochote mnacho kisiki kwa asilimia kubwa ni kazi ya akina mama kwa kazi kubwa mnyoifanya nafikiri kwa MOI mnaona wageni wanaanza kujitokeza kuizungumzia MOI vizuri ninaimani jina letu linakuwa na nitofauti na hapo zamani kwa hiyo kwa chochote mnachokisikia hapa MOI ni kwaajili ya akinamama kwani sisi wanaume tupo wachache
Ninawashukuru na kuwapa pongezi kutoka kwa Viongozi wa juu wa Serikali ninazoendelea kuzipata kupitia mimi mpaka kiongozi Mkuu wa Serikali nikwamba mnachangia kusaidi juhudi za Serikali yetu ya Awamu ya Tano inayoongozwa na MHE. Rais John Pombe Magufuli kwahiyo mnaombwa kuendelea na moyo huo huo alisema, Boniface.
Aidha alishukuru umoja huo kwa msaada huo na kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Serikali za kupunguza changamoto kwa jamii hasa upande wa afya.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Tabu Mambo (wa pili kushoto) akisalimia na kuzungumza jambo kabla ya kukabidhi misaada mbalimbali ikiwemo madawa, vyakula na vifaa tiba katika hafla fupi iliyofanyia Taasisi ya Mifupa MOI leo Machi 6, 2020 katika kuelekea siku ya Wanawake Duniani ambapo kitaifa itafanyika Mkoa wa Simiyu Machi 8, 2020. kuanzia kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake TUGHE kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) Rosemary Aaron, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Boniface na Mshereheshaji Elizabeth Mlindoko.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Tabu Mambo akizungumza jambo kabla ya kukabidhi misaada mbalimbali ikiwemo madawa, vyakula na vifaa tiba katika hafla fupi iliyofanyia Taasisi ya Mifupa MOI katika kuelekea siku ya Wanawake Duniani ambapo kitaifa itafanyika Mkoani Simiyu Machi 8, 2020. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Boniface na Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake TUGHE kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) Rosemary Aaron
Katika kukabiliana na Virusi vya CORONA wakiimba wimbo wa Chama chao bila kushikana mikono kama ilivyo zoweleka
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Tabu Mambo akimkabidhi moja ya misaada Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa MOI Dkt. Respicious Boniface
Picha ya Pamoja wakiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa MOI Dkt. Respicious Boniface
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇